Pages

Friday, September 6, 2013

MWANAMUZIKI DAZ BABA ACHANGANYIKIWA, AFANDE SELE ADHIBITISHA HALI HIYO.

Mwanamuziki Daz Baba ambaye amewahi kutamba na wimbo wa Figure Number 8 anadaiwa kuchanganyikiwa sababu za wazi zikiwa bado kujulikana. Daz Baba anadaiwa kuonekana mitaa ya Morogoro hivi karibuni huku matendo anayofanya yakidaiwa kutokuwa rahisi kufanywa na mtu mwenye akili timamu. Rafiki wa karibu wa mwanamuziki huyo wa Kundi la Daz Nundaz akizungumza na bongo5 alisema "Hivi juzi juzi Daz alikwenda nyumbani kwa Afande Sele usiku, akapiga kelele sana, Afande akaamka na kumkuta Daz akiwa mchafu na akiongea maneno ambayo hayaeleweki. Baadaye alitaka kumfanyia tendo baya mfanyakazi wa kike wa Afande lakini hakufanikiwa, ila watu wakajua kweli Daz hayuko sawa"

Nae Afande Sele alipotafutwa na Bongo5 alikiri hali ya Daz kutokuwa nzuri na kusema ameshamtaarifu Dada yake Daz aliyeko Dar es salaam kuhusu hali hiyo "Kweli hali ya Daz ni mbaya sana nimejaribu kumweka sawa lakini nimeshindwa labda wakamfanyie ,matambiko ya kwao kwasababu baba na mama yake walifariki na walikuwa hawaelewani labda kuna matatizo ya kifamilia" alisema Afande Sele ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini.

                                                       Daz Baba
 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood new

No comments:

Post a Comment