Mwakilishi wa Tanzania katika
mashindano ya Urembo ya Dunia, Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lymo,
ameondoka nchini leo kwenda nchini Indonesia katika kambi ya Miss World
2013. Pichani juu ni Brigitte akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jioni hii tayari kwa safari
hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari
muda mfupi kabla ya kuondoka nchini akiwa uwanjani hapo Brigitte
ameahidi kufanya vyema katika mashindano hayo huku akiwaomba watanzania
kumpa suport kwa kumpigia kura pindi zoezi hilo liytakapo anza kupitia
tovuti ya Miss World.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss
Tanzania, kupitia kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga
akimwelekeza machache mrembo huyo kabla ya kuondoka.
Lundenga akizungumza huku Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfed na mama yake wakisikiliza.
Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege hii leo.
Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege hii leo.
Mama na Mwana....Miss Tanzania akilamba picha na mama yake kabla ya kuruka kwenda Indonesia hii leo. SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG
No comments:
Post a Comment