Pages

Monday, September 2, 2013

LULU AWAZIBA MDOMO WABAYA WAKE KUFUATIA UZINDUZI WA FOOLISH AGE KUFANIKIWA.

Kufuatia uzinduzi wa filamu ya Foolish Age kufanikiwa na Lulu kutawala media takribani wiki nzima inadaiwa star huyo mwenye mvuto kwenye media na kwa mashabiki amewaziba mdomo baadhi ya wabaya wake walodhani nguvu yake ya awali imekwisha baada ya kukumbwa na masahibu yalompekeka segerea. Akizungumza na Swahiliworldplanet star mmoja wa kike ambaye ameshacheza filamu kadhaa na Lulu huko nyuma alisema kuwa Lulu ni mwanamke jasiri  licha ya kuwa na umri mdogo bado na kwa yaliyompata Lulu kufuatia kifo cha muigizaji mwenzake Steven Kanumba basi angekata tamaa kama angekuwa mtu mwingine.

"lazima nimpongeze Lulu kwa kuwa jasiri ameonyesha kuwa ukimuamini mungu unaweza kila kitu, pia kampuni ya Proin Promotions ni ya kupongezwa kwa kutambua uwezo wake kisanii na sio maisha yake yanayoripotiwa kwenye media, wabaya wake yamewashuka shuuu!, big up mama Lulu na mama Kanumba kwa kumpa Lulu nguvu pia" alisema star huyo.

Uzinduzi wa filamu ya Foolisha Age ulifanyika juzi tarehe 30 Mlimani City, Dar es salaam na kuhudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo wasanii wa filamu. Na kwasasa inadaiwa Lulu tayari anaigiza filamu nyingi kama mwanzoni na nyingine tayari zimekamilika zitaanza kuingia sokoni muda wowote.
 Elizabeth Michael(Lulu)

Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood new

No comments:

Post a Comment