Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na mtandao wa
habari za filamu wa filamucentral inapenda kutambulisha kwenu Tamasha la
filamu linaloitwa Dar Filamu Festival (DFF) 2013 litalofanyika katika
uwanja wa CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama, kuanzia tarehe 24- hadi 26,
September,2013 Tamasha litaambatana utoaji wa Semina kwa wadau wa
filamu, kuonesha filamu za kitanzania kwa watu wote bure kwa siku
tatu.Kutakua na filamu nne kwa siku kuanzia saa kumi na mbili jioni
mpaka saa tano usiku.
Tamasha hilo limelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona
filamu za kitanzania na zile zinazotumia Lugha ya Kiswahili pekee ili
kutoa fursa ya ajili kwa vijana na jamii husika kwa ujumla, filamu
zitakazoonyeshwa ni zile zinazotengenezwa na hapa nchini katika
kutangaza Lugha yetu nzuri ya Kiswahili kupitia kazi zao ikiwa kampeni
ya filamucentral kuitangaza lugha hiyo na kuwa ni bidhaa muhimu
Ulimwenguni.
Kwa tamasha hili la awali tutaonyesha filamu za hapa Tanzania
pekee ikiwa ni utambulisho wa Dar Filamu Festival kwa mara ya kwanza
kwenu wanahabari, miaka ijayo Tamasha litahakikisha linashirikisha
filamu kutoka sehemu mbalimbali zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutoka
popote Ulimwenguni.
Akiongea na Waandishi wa Habari mratibu wa Tamasha hilo Staford
Kihore pia amesema kuwa katika kuzingatia maendeleo ya tasnia ya filamu
siku tatu hizo kila siku imepewa jina kwa filamu zitakazoonyeshwa Tarehe
24th September, 2013 siku ya Jumanne ambayo ndio siku ya ufunguzi
utakuwa ni usiku wa Bongo Movie Classics, 25th September, 2013 ni usiku
wa Quality Nights.
Na ile siku ya mwisho tarehe 26th September, 2013 itakuwa ni
Stars Nights siku ambayo kutakuwa na wasanii wetu mbalimbali ambao
wanajenga soko hilo la Bongo movie filamu, Tamasha hili linapambwa na
wasanii wote wakiwakilishwa na wasanii wenzao wawili ambao ni Vincent
Kigosi ‘Ray’ kama Official Producer and Director for DFF 2013 na
Elizabeth Michael ‘Lulu’ kama Official Actress for DFF 2013.
Pia tamasha litaambatana na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu
kwa asubuhi ambapo madarasa yataendeshwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Idara ya Sanaa tarehe 24 September, 2013 masomo ya Uandishi wa Muswada,
Uigizaji na Uongozaji wa filamu yatafundishwa kwa washiriki, 25th
September 2013 Siku nzima Makapuni ya Utengenezaji filamu yataonyesha na
kutangaza kazi zao kwa wadau mbaliambali.
Tarehe 26th September 2013 ni siku muhimu sana kwani Taasisi
kama vile TRA, Bodi ya Ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza,
Wasambazaji wa filamu na taasisi nyingine watakutana katika jukwaa la
majadiliano kuhusu mustakabali wa tasnia ya filamu, pia filamu kadhaa
zitaonyeshwa na kujadiliwa na wadau watakaokuwepo matukio yote ya
asubuhi yatafanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa.
Pia tunatoa shukrani kwa taasisi za Serikali kutuunga mkono
katika ufanikishaji wa tamasha hilli la Dar Filamu Festival (DFF) 2013,
taasisi kama Bodi ya Filamu na ukaguzi wa michezo ya kuigiza Tanzania,
Fine Perfoming Art – Udsm, Tanzania Film Federation (TAFF), MFDI,
Swahiliwood na makapuni ya usambazaji wa filamu Steps Entertainment Ltd,
Leo Media na kampuni mpya ya usambazaji ya Proin Promotion ambayo
imeanza hivi karibuni na kuonyesha dhamira ya kusaidia tasnia ya filamu,
pia leo tunazindua mtandao wa www.dff.or.tz
Kwa kutambua mchango wako kama mwanahabari tunaamini utaungana
nasi katika kuhakikisha DFF inakuwa ni chachu ya maendeleo ya tasnia ya
filamu Tanzania, huku tukisema kuwa Dar Filamu Festival2013 kwa kauli
mbiuya ‘Ubora wa Filamu Zetu’ ikiwa ni njia ya kuwakutanisha wadau wote
kwa pamoja na kuwa jukwaa linalojenga tasnia ya filamu inayokua kila
siku. Pia tunaomba ushiriki wako katika kufanikisha hili.
Imetolewa na Mratibu wa Tamasha la DFF 2013 Staford Kihore.
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood new
.
No comments:
Post a Comment