Mastaa wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) na Slim Omar wamenaswa katika
maeneo ambayo ni ngumu kuwakuta wawili hao.
Mwanzoni ilidhaniwa wanarekodi filamu ila waliposogelewa ikagundulika hapakuwa na
kamera yoyote katika eneo walilokuwepo kitu ambacho kilizua maswali mengi. kwa mujibu wa thesuperstarstz Slim alikuwa akimsomesha Batuli ili akubaliane na alichokuwa akimueleza japo mwandishi hakufanikiwa kujua alikuwa akimsomesha kitu gani huku wenyewe mwanzoni wakiwa hawajui kuwa wanafuatiliwa na paparazi ambaye alifanikiwa kuwapiga picha bila wao kujua.
Baada ya hapo wawili hao walifuatwa na walipojua kuwa wanafuatiliwa wakaachiana mikono haraka na kuangua kicheko huku Slim akionekana kutoamini kuwa wamebambwa na kisha wakaondoka haraka eneo hilo. Walipoulizwa kulikoni, wawili hao hawakutoa ushirikiano wowote. Hata hivyo habari za chini chini ni kuwa mastaa hao wa filamu wanapendana ingawa hawajaweka wazi na inadaiwa hawapendi kufuatiliwa na mapaparazi na wiki kadhaa nyuma swahiliworldplanet iliwahi kuwauliza baada ya kudaiwa ni wapenzi kwa siri lakini wote walikana madai hayo. Batuli na Slim wamecheza pamoja filamu ya Waves Of sorrow wakiwa na Ray na Rose Ndauka na pia filamu mpya ya Coast 2 Coast inakuja huku waigizaji wakuu wakiwa ni batuli na Slim. Angalia picha chini jinsi wawili hao walivyobambwa.
|
Hapa ni mwanzo Batuli alionekana kufurahia maneno ya slim |
|
Hapa inaonyesha Slim aliongeza utamu wa maneno na kumfanya Batuli aanze kuingia mkenge kwa maneno yake. |
|
Duh...tumebambwa! mapaparazi noma kweli. | | | | | | | | | | |
|
Follow us on twitter
Swahili World Planet and Like our facebook pages
Swahili World Planet and
Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood new
Waandishi ni noma halafu eneo zuri sijui wapi hapo Slim Kama unampenda Batuli muoe mnaendana sana.
ReplyDelete