Habari ni kuwa Jumatano iliyopita watu walijaa pomoni katika mahakama ya mwanzo Kawe jini Dar es salaam kwa lengo la kusikiliza kesi ya Wema Sepetu na pia kumuona actress huyo ambaye anakabiliwa na kesi ya Kushambulia, kufanya vurugu, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao meneja wa hotel Goodluck Kuyumbu. Wema aliyepandishwa kizimbani mbele ya hakimu Bernice Ikanda alifika mahakamani hapo akiwa na msafara wa magari matatu yaliyokuwa na wapambe wake kwa mujibu wa GPL. Magari hayo matatu yaliyokuwa yamejaza wapambe wa star huyo yalikuwa ni aina ya Audi Q7, Toyota Opa na Toyota Hiace. Kesi hiyo iliahirishwa mpaka August 20 mwaka huu itakaposikilizwa tena. Angalia picha............
Like our facebook page Swahili World Planet
for more updates about Swahili movies' latest news, gossip,
celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood
news
No comments:
Post a Comment