Pages

Friday, August 9, 2013

ROSE NDAUKA NA LUCY KOMBA WAMCHUNIA MONALISA.

Rose Ndauka
Mastaa wa filamu  Lucy Komba na Rose Ndauka wanadaiwa kumchunia msanii mwenzao Yvonne Cheryl (Monalisa) kisa kikitajwa kuwa ni prodyuza Mghana aitwaye Prince. Chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kikizungumza na globalpublishers kilidai kuwa awali Monalisa na Prince walikuwa washikaji na baadaye Monalisa akamtambulisha Lucy kwa jamaa huyo na hapo ndipo tatizo lilipoanzia. Chanzo hicho kilifunguka kwa kusema.....


"Lucy alipojuana na Prince akamchukua Rose kisha wote watatu wakaenda Ghana eti kushuti filamu. Wakiwa huko sijui walimwaga sumu gani na hapo ndipo uhusiano wa Mona na Prince ulipoanza kufifia.
“Mona akashangaa ila akapotezea na hata Lucy na Rose waliporudi hawakuwa wakimchangamkia mwenzao, wakaanza kumchunia mpaka sasa" 


Baada ya kuzipata nyeti hizo, mwandishi alimtafuta Monalisa ambaye alipopatikana alikiri kuwepo kwa ‘mnuno’ kutoka kwa wasanii wenzake hao, akasema chanzo ni Prince.
"Niliamua kuachana na Prince kwa kuwa niliona ana tamaa na wasanii na nashangaa Rose na Lucy nao wanavyonichunia, ingawa kiukweli sikupenda kabisa kuongelea suala hili kwani sipendi shari" alisema Monalisa.
Rose alipoulizwa alikuja juu na kudai hajawahi kuwa na ukaribu na Monalisa. Lucy hakuweza kupatikana kufungukia madai hayo.

                                                                   Monalisa
  Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment