Pages

Saturday, August 3, 2013

SIVAI TENA HERENI KWENYE FILAMU ZANGU: HEMED

Suala la kuvaa hereni kwa waigizaji wa kiume katika filamu kwenye scenes ambazo haziruhusu pambo au urembo huo limekuwa kero kwa baadhi ya filamu na waigizaji ambao huonekana wazi lengo lao ni kupendeza au kuuza sura na sio kuvaa kuendana na scenes zinavyotaka. Baadhi ya waigizaji wa kiume Swahiliwood ambao wamekuwa wakiongoza kwa kuvaa hereni sehemu zisizostahili katika filamu na kuishia kuharibu ni pamoja na Hemed Suleiman na Vicent Kigosi(Ray). Suala hilo tumekuwa tukiliandika sana hata hapa Swahiliworldplanet na suluhisho zake ingawa wengine bado wameziba masikio. Hata hivyo Hemed tayari ameshaona kosa lake na kuamua kuacha. "kumekuwa na fight kubwa sana kati yangu na director wangu pale ninapokuwa na scenes za ofisini nakuwa mbishi sana suala la kuvaa hereni sasa nimepata ushauri toka kwa mashabiki wangu nimeona nikamshauri director wangu kuepuka kero ambazo hawazipendi mashabiki wangu, nitakuwa mjinga nisipowasikiliza mashabiki wangu" Hemed ambaye pia ni mwanamuziki aliambia E-NEWS ya East Africa Tv.

Kutokana na maelezo ya Hemed hapo juu ni wazi kuwa baadhi ya waigizaji wanavaa ili kupendeza tu na sio kuendana na uhusika na pia wao huwa waamuzi wa mwisho kwa kila kitu pasipo director kuwa na nguvu anapomuongoza msanii kitu ambacho ni udhaifu kwa waongozaji wa namna hii kuacha kazi iharibiwe na mtu na kubaki kuwa muongozaji pambo tu. Na kwa wale waigizaji ambao pia huongoza filamu zao wenyewe basi wao ni rahisi kuendelea na hali hii kwa kuwa wao ndiyo wenye sauti ya mwisho na ushauri kwao ni mwiko huku wakionekana wazi kuvurunda na kulipua kazi katika mavazi na make up.

Ushauri ni kuwa hata uwe mtaalam vipi lakini duniani watu hujifunza kila siku hivyo kupokea ushauri unaojenga ni kitu muhimu katika maendeleo ya filamu zetu. Na pasipo hivyo basi mwisho wa siku hata filamu zitakosa soko kutoka kwa mashabiki na wanunuzi. Hongera Hemed kwa kulikubali kosa lako na kuamua kufuata ushauri wa mashabiki

                                                      Hemed
 Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment