Mtangazaji wa radio Victoria fm iliyopo Musoma mkoani Mara Patrick Derrick Mwankale a.k.a The International boy ambaye anaendesha vipindi mbalimbali, kikiwemo kipindi cha burudani cha Strengo Saturday kinachorushwa kila jumamosi saa tano asubuhi hadi saa nane mchana ameamua kuandaa shindano la kumtafuta mkali chipukizi upande wa kuimba na kurap. Mshindi wa shindano hilo atapewa tuzo na zawadi nyinginezo zikiwemo nafasi za kurekodi na kufanya video katika studio kubwa zinazotambulika hapa nchini. Form za kushiriki shindano hilo bado zinaendelea kutolewa na zinapatikana radio Victoria fm na kwa wale walio mbali ambao wangependa kushiriki ili kupata maelezo zaidi basi wasiliana na Mtangazaji huyo mahiri hapa Mkali wa kuimba na kurap Musom, Mara. Form zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu 5000 tu na mwisho wa kuchukua form ni tarehe 10 mwezi huu wa nane hivyo wahi ili kutimiza ndoto yako ya kushine kwenye game la music wa Bongofleva.
Patty ambaye ni muandaaji wa shindano hilo na mtangazaji wa Radio Victoria fm
Like our facebook page Swahili World Planet
for more updates about Swahili movies' latest news, gossip,
celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood
news
No comments:
Post a Comment