Pages

Sunday, August 25, 2013

RIYAMA ALLY AFUNGUKA MADAI YA KULETA USUMBUFU NA MTOTO WAKE KAMBINI.

Muigizaji maarufu nchini na anayekubalika kwa wengi Riyama Ally anadaiwa kuanza kulalamikiwa na baadhi ya waongozaji wa filamu nchini kuwa baada ya kujifungua amekuwa akileta usumbufu usio wa lazima katika utengenezaji wa filamu anazocheza kwa kwenda kambini na mtoto wake na linapokuja suala la malazi anataka kupewa chumba yeye, baba mtoto wake na mlezi wa mtoto wake. Na hataki kulala pamoja na wasanii wenzake. Habari hizo ziliripotiwa wiki iliyopita na juzi zilifika hapa SWP kwa mmoja wa waandaaji na muongoza filamu kulalamikia kitendo cha Riyama kuwa kinaweza kumpoteza kisanii kama asipochukua tahadhari mapema. "Riyama anatakiwa aangalie upya uamuzi wake wa kwenda location na familia yake na kutaka kuongeza budget ya producers bila ulazima wowote la sivyo anaweza kupotea kisanii" alisema muongozaji huyo aliyekataa kutajwa jina lake

Baada ya kupata habari hizo ilibidi kumtafuta Riyama na alipopatikana alisema alikuwa busy kwa muda huo na simu yake haikuwa na chaji ila angejibu usiku na kweli ilipofika usiku juzi Riyama alijibu kwa kusema "walitaka niende na nani kambini??? haya ni maisha yangu naishi niwezavyo siishi nitakavyo....wakiniona mzigo waniache!, Najua wanataka kunichafua ila mungu hatasimama nao atawalipa kwa vizazi vyao inshallah". Actress huyo mwenye filamu nyingi sokoni aliongeza kwa kusema "maneno yao si mkuki na ndio maana wasemayo sishituki...wao wakosefu zaidi yangu pengine.... nawaheshimu tu namuogopa mungu tu"

Hata hivyo tunadhani hali hiyo imesababishwa na Riyama kuhitajika katika filamu nyingi azicheze huku mwanae bado akiwa mdogo hivyo baada ya muda mchache ujao atakuwa kama zamani kwa kuwa haijawahi kuripotiwa huko mwanzo habari kama hizi.

 Like our facebook pages Swahili World Planet Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment