Mtitu ambaye ni muigizaji maarufu na wa siku nyingi, pia director na producer ambaye ameibua vipaji vingi Swahiliwood ameandika hivi katika mtandao mmoja wa kijamii leo "
"OMEGA, historia mpya…
Leo tumeanza kuisambaza filamu yetu ya OMEGA na imepokelewa vizuri
kiasi cha kutulazimu kuzalisha upya nakala nyingine masaa matano tu
baada ya kuiingiza sokoni.
Nilipotangaza kujikwamua kutoka katika
makucha ya wanyonyaji kwa kuanza kusambaza mwenyewe sinema zangu
nilipokea kashfa nyingi sana kutoka kwa wasanii wenzangu hasa mastaa
kuwa nitashindwa lakini sikurudi nyuma, nilikaza moyo na kuendelea na
mkakati wangu.
Naomba watanzania wenzangu muendelee kuniunga mkono ili hata wenzangu wapate ujasiri wa kujikomboa.
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru watendaji wote wa 5 Effects,
waandishi wa habari, baadhi ya viongozi wa serikali, marafiki wa ndani
na nje ya nchi kwa kuwa nami bega kwa bega katika uamuzi huu mgumu.
AHSANTENI SANA WATANZANIA WENZANGU KWA SAPOTI YENU.
By
William Mtitu"
Like our facebook pages Swahili World Planet Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.
No comments:
Post a Comment