Pages

Saturday, August 24, 2013

NORA KUJA NA KIPINDI CHAKE CHA TV.

Muigizaji maarufu nchini Nuru Nassor(Nora) anakuja pia na kipindi chake cha Tv. Akizungumza na Starehe Nora alisema kuwa kwa sasa yupo katika mipango ya kusajili kipindi chake kabla ya kuchagua kituo ambacho atakuwa akirusha matangazo yake. Nora kwasasa anatamba sokoni na filamu ya Msimamo Wangu na filamu yake nyingine ya Ndoa Goli La Tatu inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Nora ni muigizaji wa siku nyingi ambaye alitoa hamasa kwa wasanii chipukizi na kuingia kwake kwenye Tv atakuwa amefuata nyayo za mastaa wenzake kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, Rose Ndauka na wengineo.

                                                   
Nora
 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment