Saturday, August 31, 2013

LICHA YA KUFANYIWA HUJUMA MTITU AFANIKIWA SOKONI NA FILAMU YA OMEGA CONFUSION.

William Mtitu ambaye ni producer na msanii maarufu Swahiliwood baada ya kuwekewa vizingiti katika kazi yake ya usambazaji wa filamu amesema anamshukuru Mungu kwani ameishinda vita hiyo. Mkurugenzi huyo wa kampuni ya 5EFFECTS kabla ya kufanikiwa kusambaza filamu yake ya Omega Confusion ambayo amecheza na Irene Uwoya iliyotoka Jumatatu iliyopita inadaiwa kwamba kampuni moja maarufu ya usambazaji wa filamu nchini ilimwekea vizingiti kwa kutoa filamu kila siku ambazo Mtitu alitangaza kuitoa kwa mara ya kwanza filamu hiyo..
"Najivunia kwamba nimeshinda vita maana jamaa walikuwa wakinifanyia mchezo mchafu. Kila nilipotangaza kutoa filamu na wao wakawa wanaingiza filamu mpya lakini nashukuru Mungu kwamba sasa hivi nimeweza.
Huwezi kuamini, nilipoingiza sokoni Omega ndani ya masaa matano nililazimika kuongeza nakala nyingine kwani inanunuliwa kama karanga" alisema Mtitu

Muigizaji na producer huyo ambaye ameibua vipaji vingi hivi karibuni aliweka wazi kuwa amechoshwa na unyonyaji wa baadhi ya wasambazaji kwa wasanii hivyo kuamua kuanza kusambaza kazi zake mwenyewe. Na kitendo cha filamu hiyo kufanya vizuri sokoni ni wazi kuwa wasanii wengine wanaolalamikia kunyonywa wataanza kuamka pia na kuchukua hatua stahili kama Mtitu.

Mtitu na Irene Uwoya wakiwa katika moja ya scenes za filamu hiyo.

 Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment