Pages

Friday, August 2, 2013

FLORAH MVUNGI USITUITE WANAFIKI UNAKOSEA SANA: BATULI

Actress maarufu nchini Yobnesh Yusuph(Batuli) ameipinga kauli ya wanandoa ambao pia ni wasanii maarufu nchini Florah Mvungi na H.Baba baada ya wawili hao kuhojiwa katika kipindi cha Take One kinachorushwa Clouds Tv hivi karibuni na kusema kuwa harusi yao haikuhudhuriwa na mastaa wengi wa filamu kwa kuwa industry hiyo imejaa watu "masnitch". Walisema hata kama walialika wachache lakini ambao hawakualikwa pia wangeweza kuhudhuria. Lakini akijibu tuhuma hizo ikionekana pia kama kwa niaba ya waigizaji wengine ambao hawakuhudhuria harusi hiyo  Batuli aliyejaaliwa mvuto wa aina yake aliandika "Florah Mvungi usitulaumu, usituite wanafiki ni neno baya sana. tumewachangia wangapi? kwanini wewe tusikuchangie? ulialika uwatakao usilalamike"

"Mr & Mrs. H.Baba napinga kauli ya kusema ndoa sio mpaka ualikwe jamani hivi kweli kabisa nivae gauni langu niende ukumbini sijaalikwa" aliongeza Batulli

                                            Batuli
 Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

8 comments:

  1. Yaonyesha Flora ba H baba hawakutaka support wenyewe ubaguzi wa kuwathamini baadhi ya wasanii utakuwa umemfunza kwenye mahojiano aliwataja aliowaalika na sisi mashabiki tulisikia sasa analalamika nini? Flora na mumeo watakeni radhi bongo movie.

    ReplyDelete
  2. Achaneni nae kachemsha ukiwadharau wenzio faida yake ndio hiyo Aunt Ezekiel alichangiwa na bongo movie na harusi ikawa na dubai wakaenda kwako kwanini usichangiwe? Angalia ulipojikwaa Flora punguza lawama na uisafishe bongo movie kwa hili umekosea usiseme wanafiki wakati hukuwapa nafasi na heshima yao.

    ReplyDelete
  3. Flora kaa chini uombe mola uzae salama pia jisitiri clouds tv ulionekana ukiwa hujavaa kama mke wa kiislam lile jina ulilojidai nalo hadhi yake ni kubwa kwenye dini ya kiislam bi khadija hakuwa anatembea utupu pili watake radhi wenzio jifunze kushirikiana nao sio kugombana nao. Naitwa Khadija Suleiman

    ReplyDelete
  4. Shit umewakosea unawaitaje wanafiki? Mpaka batuli kajibu bhasi haupo sawa. Edward

    ReplyDelete
  5. Star ana maneno ya hekima huyu mpaka raha be blessed love tunakupenda mpaka basi flora hajui maandalizi mumsamehe bure karibu dodoma batuli wa bosco

    ReplyDelete
  6. Mpaka bubu kaongea hii mpya Batuli huwa haongeagi jamani atakua kaumia kwa kuitwa wanafiki hey flora and your hubby say sorry

    ReplyDelete
  7. Florah chunga sana hilo domo lako

    ReplyDelete
  8. Jifunze Flora acha uzuzu

    ReplyDelete