Pages

Monday, August 5, 2013

BATULI NA SLIM OMAR WAFUNGUKA BAADA YA KUDAIWA KUWA WAPENZI KWA SIRI.

Kuna tetesi za chini chini kuwa waigizaji maarufu nchini Yobnesh Yusuph(Batuli) na Slim Omar ni wapenzi na uvumi huo kufika mpaka hapa Swahiliworldplanet. Chanzo cha habari kikizungumza na SWP jana kilisema " hivi mnajua kuwa Batuli na Slim Omar wapo katika dimbwi la mapenzi lakini sijaona habari popote mpaka sasa, Shauri yenu mwaya mnapitwa na habari na Batuli ameandika mpaka twitter kuwa anampenda Slim na pesa haina nafasi kwake, ingia twitter ujionee ingawa umechelewa kidogo kujua". Baada ya kupata habari hizo jana ilibidi kuingia twitter na kweli katika akaunti ya Batuli kulikuwa na picha ya Slim Omar hiyo iliyopo hapo chini na kuambatana na maneno yaliyosema " I think i'm in love... i don't care about money". Picha na maneno hayo viliwekwa katikati ya mwezi July mwaka huu.  Baada ya kupata habari hizo ilibidi

Batul
 Swahiliworldplanet kuwatafuta mastaa hao jana hiyo hiyo na wa kwanza kupatikana alikuwa Batuli na alipoulizwa alisema "That is a very hard answer  to your very hard questions...watanzania wasubiri siku yangu kubwa iliyopangwa na Mwenyezimungu, itakuwa ni siku nitakayoitwa mke kwa yule nitakayejaaliwa nae. Nimelelewa kimaadili na nje ya yote nazijua tamaduni za nchi yangu ya Tanzania. Sijawahi kutangaza kuwa nina mwenza wakati ukifika wa mimi kuolewa ndiyo nitatangaza so I don't think I have a chance with him. Mashabiki wangu nawaomba wawe na subira siku yangu ikiwadia basi mwenza wangu watamjua. Najitambua na naheshimu mila zetu". Star huyo alipoulizwa kama yupo single au ana mtu kwasasa alisema kuwa yupo single.

Slim Omar
Baada ya kupata maelezo ya Batuli ilibidi kumsaka Slim Omar ambaye pia kwasasa anafanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini na alipopatikana na kuelezwa kuhusu kuwa wapenzi yeye na Batuli alijibu "Hapana, Batuli ni mtu ninayefanya nae kazi kwa uzuri na ushirikiano wa hali ya juu na katika movie yangu ya Coast 2 Coast, hakuna kingine na kama aliniandika ni kwa uzuri tu wa kawaida kama wasanii tunaotegemeana katika kazi zetu"

Hata hivyo picha hiyo ya Slim iliyoambatana na maneno hayo hapo juu leo haikuonekana tena ikionekana Batuli kaiondoa baada ya kuanza kuleta kizazaa. Kama upo twitter basi follow the actress hapa BATULI ili kupata updates zake.

Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

16 comments:

  1. Hapana my model hawezi kuwa na Slim. Batuli nakupenda kama vipi tuwekee wazi tujue muhusika ni nani. Mimi Anitha

    ReplyDelete
  2. Bonge ya couple kwa kweli muoane mtapendeza mno. Jasmin

    ReplyDelete
  3. I wish niwape zawadi watazaa watoto wazuri halafu wote wazuri goooooosh karibuni Arusha its me Gerald

    ReplyDelete
  4. Zoom zoom zoom kama siamini amini congratulations brother Slim oa fastaaaaaaaaaaaaaaaaa michango tutakupa mwanaume huwa hafikirii mara 2 weka ndani jumlaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  5. Bhaaa bhaaaaa bhaaaaa WW SLIM HUJITAKII MEMA HAO NI WAKE WA VIONGOZI UTAKUFA KWA MRESHA BURE huna hela ya kumiliki hii ngoma; SEIF

    ReplyDelete
  6. Mungu awe nanyi TUNASUBIRI KADI ZA MICHANGO

    ReplyDelete
  7. Makofi kwenuuuuuuuuu uamuzi wa busara qote vijana mfunge ndoa sasa

    ReplyDelete
  8. MIND YOUR OWN BUSINESS SEIF DONT TALK SHIT MWANAUME FALA KAMA WW NDIO HAJIAMINI UZURI WA MWANAMKE NI MOYO WAKE SIO SURA YAKE WALA UMBO DO YOU THINK BATULI NI KAMA HAO MAKAPU YA SOKONI MAKE SURE UNAONGEA KITU UNACHOKIJUA NAMKUBALI SANA HUYU DADA ANANIDHAMU KAMA RIYAMA SIJAWAHI KUSIKIA CIVIL MBAYA KABISA MUACHE SLIM AOE MUNGU ATAWAPA NGUVU NA ULINZI WAMEUA NA WATAWEZA UKITAKA KUTAMBUA UMEOA JIWE CHUNGUZA INTERVIEW ZA HAWA MASTAR ONA ALIVYOJIBU HAPO JUU KAPANGUA NA KAJIBU KINIDHAMU HAWEZI KUTANGAZA ANAZINI WAKATU ANAJUA MILA ZA KITANZANIA NA DINI INAKATAZA KASEMA WAKATI UKIFIKA ATATANGAZA NDOA. DONT SPEAK LIKE A DEVIL SEIF I'M CHRISS FROM KAHAMA

    ReplyDelete
  9. NAWAPA MUKONO YA BARAKA MUJE NA BURUNDI HONEYMOON MUKUJE MUFANYE KULE MUDADA NI MUZURI HUYU BATUL BATUL BATUL MUMACHO YA KWAKE SASA

    ReplyDelete
  10. Duh nimeipenda, pia ni kati ya kina dada ninaowakubali sana katika film industry tanzania

    ReplyDelete
  11. Nimependaaaa Slim njoo ubebe michango yako huku Zanzibar Oa Sheikh OaAaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  12. Pongezi zangu za dhati ziwafikie nyie 2 mmeamua kitu kizuri ndoa uwe mapem jaqline sewawa

    ReplyDelete
  13. Hii blog tamu sana ina mambo kemkem hii inaitwa Breaking News tunawasubiri

    ReplyDelete
  14. Majanga majanga majangaaaaaa weye slim utakufa kwa kihoro weyejitie tashtiti uone wamuezea wapi hiyu bi batuli mzuri mno huogopi weye? Wallahi uone vinginevyo uhawara watakuhawaria shauri yako ivoooo mke mzuri kama katerenshwa yalaaaaah una makubwa weye sikuwezi muweke ndani haraka wajanja wasimpose juu kwa juu fanya hima ivooo mie sadiq yule rafikiyo wa zenzi mlipokuja kushutiii tena na batuli ulikija nae watoto mnasiri nyie heeeeh inshaallah kila la kheri

    ReplyDelete
  15. DADA BATULI SALI SANA KWA MUNGU WAKO UMEUMBIKA MAMA MZURI SANA SANA SANA SIJUI KAMA UMEWAHI KULIONA HILI WEWE NO MWANAMKE KATIKA WANAWAKE UNA MVUTO SANA UKIJUMLISHA NA NIDHAMU YAKO MBELE YA JAMII NDIO KABISA JIPENDE DADA WEWE NI MZURI MIMI NI MWANAMKE MWENZIO MPAKA NIMEKUAMBIA HIVI NIAMINI UNAMVUTO SANA SANA SANA NAITWA MAZNAT

    ReplyDelete
  16. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete