Pages

Thursday, August 8, 2013

BATULI AMUANDIKIA UJUMBE RAIS KIKWETE KUMUOMBA ALIVUNJE BASATA.

Yobnesh Yusuph(Batuli) ambaye ni actress maarufu Swahiliwood amemuomba Rais Jakaya Kikwete alivunje Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) na kuliunda upya. Leo kupitia akaunti yake ya twitter muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto na kupendwa na mashabiki wengi wa filamu ali-tweet moja kwa moja akimtaja JK kwa kuandika "ujumbe wa sikukuu ya Eid kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vunja baraza la BASATA uliunde upya".

Ingawa Batuli hakutaja moja kwa moja kwanini baraza hilo linalosimamia sanaa ikiwemo tasnia ya filamu nchini livunjwe lakini kwa muda mrefu wasanii wakiwemo wa filamu na muziki wamekuwa wakililalamikia baraza hilo kuwa linafanya mambo kienyeji na baadhi ya wasanii kudai kukumbana na urasimu wanapotaka kufanya kazi zao za sanaa. Wengine wanadai hata hatua iliyopigwa sasa katika sanaa nchini ni juhudi za wasanii wenyewe pasipo sapoti ya kutosha kutoka BASATA. Baadhi ya wasanii wa filamu wamekuwa pia wakitaka TAFF ndiyo ipewe mamlaka kamili ya kusimamia shughuli zote za tasnia ya filamu nchini kutokana na BASATA kuwepo muda mrefu lakini Sanaa ya Tanzania bado haijapewa hadhi ya sekta rasmi na kuwa na sera ya kueleweka katika kumkomboa msanii na kuzidi kupiga hatua.

 Hivi karibuni pia mwanamuziki Diamond Platinumz alikaririwa akisema BASATA ndiyo wa kulaumiwa kwa kutokuwa na tuzo nyingine za muziki mpaka sasa kwakuwa chombo hicho kimekuwa kikiweka kauzibe kwa watu wanaotaka kuazisha tuzo mbalimbali za sanaa ikiwemo hata katika tasnia ya filamu.

 Kama wewe ni shabiki wa Batuli basi m-follow hapa BATULI-ACTRESS katika mtandao wa twitter ili kupata updates zake


 Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

8 comments:

  1. Good girl today your talking Mrs Slim Jk vunja Basata

    ReplyDelete
  2. SAMAHANI MWENYE BLOG BATULI ANAPHOTOS NYINGI HII UNAIPENDA SANA USITUFANYIE HILA WELL POLENI WASANII BASARA YAONYESHA NI KIKWAZO KIKUBWA SANA KWENU

    ReplyDelete
  3. You are a strong woman Batuli

    ReplyDelete
  4. Keep it up girl umetupa jiwe mahala pake hamnufaiki na Basata mnaibiwa na haki miliki zenu zinamilikiwa na muhindi Mr President aache kucheka cheka sasa panga tu

    ReplyDelete
  5. BE BLESSED GIRL I LOVE THE WORDS HON JAKAYA KIKWETE SIKILIZA KILIO CHA NYOTA WETU AT THE END OF THE DAY MNAWATUMIA KWENYE KAMPENI WAFUTENI MACHOZI YAO. HUYU KAAMUA KUKUANDIKIA UJUMBECWA WAZI ON TWITTER SHE IS A STRONG WOMAN ANA MAUMIVU YA KUTOSHA UAMUZI WA KUTWEER LIVE NI MGUMU SANA NI SAWA NA MFUNGWA ALIYETUMA BARUA YA WAZI KWAKO KUPITIA GAZETI WAONEE HURUMA WASANII WETU WANAKUFA WAKIWA HAWANA KITU. MY NAME IS JAMES E. MSUYA

    ReplyDelete
  6. tatizo TZ tuna msanii sio wasanii... mnakera bwana y msifight as a team¿ midiocre

    ReplyDelete
  7. POLENI WASANII WETU KWANI BASATA NI NINI? NIELEWESHENI WACHANGIAJI WENZANGU

    ReplyDelete