Actress Yobnesh Yusuph(Batuli) ameamua kuajiri meneja wa kusimamia kazi zake za filamu katika harakati zake za kusonga mbele zaidi na kufanya kazi kimataifa. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Batuli ambaye tayari anakubalika katika tasnia ya filamu Swahiliwood ameandika "Nadhani now ni muda wangu wa kujitangaza kimataifa, nina imani nikiweka meneja atanisaidia kwa mambo mengi sana.....my time is now dua zenu kwangu pls". Ingawa bado hajamuweka wazi meneja huyo lakini muda sio mrefu atajulikana na ni uamuzi mzuri na wa kuona mbali pia.
Ni wazi kuwa waigizaji wengi wa filamu bado hawana mameneja wa kusimamia kazi zao licha ya baadhi yao kuwa na umaarufu mkubwa ambao ungeweza kuwaletea faida kubwa ikiwemo deals za matangazo ya makampuni mbali mbali lakini wanaishia kuandikwa magazetini kwa skendo tu. Meneja ni lazima aijue vizuri tasnia husika ya msanii na network ya kutosha, pia awe na uwezo mkubwa wa kumsimamia msanii ambapo kwa wenzetu mameneja wengine husomea kabisa kazi hiyo. Na pia meneja ni lazima awe na upeo kuhusu masuala ya mikataba na sheria ili kuepuka msanii kunyonywa. Meneja mzuri pia humuongoza msanii husika ajijenge na kujitegemea mwenyewe na kumuepusha na negative image hasa katika media kwa kumshauri vizuri kuwa makini na vitu vinavyoweza kumharibia sifa na heshima yake. Lakini kuna baadhi ya mameneja wa wasanii nchini wanaonekana hawana upeo katika tasnia husika ya msanii kitu ambacho si kizuri kwa maendeleo ya msanii kisanaa.
follow the actress on twitter BATULI ACTRESS
Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
Hatua nzuri Batuli
ReplyDeleteHatu nzuri madam usichoke ipo siku utafanikiwa kwa yale yote unayoyataka go girl go u will win
ReplyDeleteAll da best baby. Samira
ReplyDelete