Pages

Monday, August 5, 2013

ACTRESS IRENE UWOYA ANUNUA MERCEDES BENZ LA GHARAMA(PHOTOS).

Muigizaji Irene Uwoya kwasasa anamiliki gari jipya la gharama aina ya Mercedez Benz S Class 550 Sedan yenye rangi ya black metalic. Ingawa gharama za gari hilo analoendesha actress huyo maarufu hazikujulikana kutoka kwake mwenyewe lakini inadaiwa kuwa aina ya gari hilo likiwa jipya huweza kugharimu dola za kimarekani $ 95,000. Hivi karibuni actress huyo alikuwa nchini Swaziland ambako alikuwa na ziara binafsi na baada ya kurudi mwenyewe alisema mfalme Mswati wa Swaziland ameahidi kumsapoti katika kazi zake za filamu. Pia actress huyo tayari ameingia katika vipindi vya Tv akiwa na kipindi chake cha Paradise kinachotarajiwa kuanza Jumaanne  wiki hii Clouds Tv.

Miezi michache iliyopita actress mwingine maarufu nchini Jackline Wolper alinunua gari jingine la gharama na hivi karibuni Wema Sepetu nae aliongeza gari jingine la gharama katika list ya magari yake. Hivyo utadhani kuna mchuano usio rasmi kwa actresses hawa maarufu katika kumiliki magari ya gharama. Angalia picha za gari jipya la Irene Uwoya hapo chini............................

                                 Irene Uwoya akiwa na Benz lake
Images by: millardayo
Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment