Pages

Sunday, July 28, 2013

RAY ANAWAPOTOSHA MASHABIKI WANGU: BATULI

Actress maarufu wa filamu za kiswahili Yobnesh Yusuph(Batuli) amemshukia muigizaji mwenzake Vicent Kigosi(Ray) kwa kitendo cha kutumia majina ambayo hayapendi katika filamu zake na blog yake. Mara nyingi filamu anazoigiza Batuli kutoka Rj company jina la actress huyo huandikwa kama Nesh Mohamed au Nesh Yusuph, ukiachilia mbali hilo hata katika blog yake(Ray) Batuli huandikwa kwa Jina la Lisa wakati mwingine kitu ambacho huwa kinawachanganya baadhi ya mashabiki wa muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto wa hali ya juu. Baadhi ya mashabiki wa muigizaji huyo juzi waliambia Swahiliworldplanet kuwa wanachanganywa na majina ya ya actress huyo kwa jinsi yanavyokuwa tofauti katika blog ya Ray na filamu hasa kutoka Rj.

Hata hivyo siku za nyuma mtandao huu uliwahi kumuuliza batuli na kusema kuwa yeye anataka aitwe Yobnesh Yusuph a.k.a Batuli jina ambalo alipewa na marehemu Steven Kanumba na kulikubali pia kama ishara ya kumuenzi baada ya Kanumba kufariki. Juzi baada ya mashabiki wa muigizaji huyo kuuliza tena kuhusu majina ya Batuli kuwa tofauti ilibidi kumtafuta actress huyo hata hivyo hakupatikana ila leo tulimpata na alipoulizwa na SWP alisema "Yobnesh Yusuph ndilo jina langu halisi na la kazi ni Batuli. Ray ni kawaida yake kunivurugia jina langu ila naomba watanzania wajue Naitwa YOBNESH YUSSUPH  a.k.a BATULI. Wanaoweka Nesh Mohammed hawatumii akili, kabla ya kazi kuna mkataba wa kazi na bado ukienda kupiga picha ya cover pia kuna form unajaza pale kwa Raqey(i-view media) lakini cha kushangaza wananipa majina tofauti sio siri nachukizwa sana na upuuzi wanaonifanyia watu kila siku nafanya nao kazi lakini eti hawajui jina langu ni makusudi tu. Ray anawapotosha mashabiki wangu hawajui waniite nani"

Pia ameshangazwa na jina la mohamed kutumiwa kama jina lake la pili wakati ni jina la aliyewahi kuwa mpenzi wake zamani Nice Mohamed(Mtunisy) ambaye pia ni muigizaji maarufu nchini. " Nesh Mohammed sijui Ray alilitoa wapi maana jina la Mohammed ni la msanii maarufu nyie mnamjua kwa jina la Mtunisy ni x-wangu kwa sasa lakini cha ajabu wamelikomalia. Nesh ni kifupi cha jina langu yaani Yobnesh sasa ukiondoa Yob ndio inabaki Nesh". Kuhusu Ray kumuita Lisa alisema jina hilo alilitumia katika igizo flani enzi zile wanarusha michezo yao ITV.  kwa hiyo muigizaji huyo anataka vyombo vya habari, mitandao na katika filamu aitwe au kuandikwa kama Yobnesh Yusuph(Batuli) na hayo mengine hataki kuyasikia.

Ni muda mrefu sasa kumekuwa na tabia ya baadhi ya waigizaji au mastaa nchini kuitwa majina kibao sababu ikiwa ni magazeti ya udaku, graphic designers na editors wa filamu kutokuwa makini na majina ya wasanii na pia wasanii wenyewe kwa wenyewe kupachikana majina na baadhi kuyatumia kama utambulisho wa msanii katika kazi zake na jamii kwa ujumla huku mhusika mwenyewe akiwa hayataki majina hayo wakati mwingine na kasheshe inakuja pale msanii wa kike anapoitwa jina la mpenzi wake na kuwa maarufu halafu baadaye kuachana na kupata mpenzi mpya ambaye hataki kusikia tena mpenzi wake akiwa na jina la mwanaume wa zamani. Suluhisho la tatizo hili ni wasanii kukaa au kuita media hasa magazeti ya udaku na mitandao na kueleza majina wanayotaka yatambulike kama utambulisho wao, pia graphic designers na editors wa filamu wanatakiwa kuwa makini na majina halisi ya wasanii kwakuwa wao pia ni chanzo cha tatizo.

                                                   Yobnesh Yusuph(Batuli)
Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

3 comments:

  1. Hana lolote huyo ray roho mbaya tu mtu unafanya nae kazi kila siku na kumbe mikataba mnawasainisha roho ya kichawi tu labda anamjua chuchu hanse pole da Batuli achana nae ila hili na kudate na mtunisy booooooooonge la surprise.

    ReplyDelete
  2. Ray sikupendi sasa unafanyia hivi ili iwe nini? Binti wa watu anakutendea haki kwenye kazi zako angalia Waves of sorrow ndio utajua heshima ya huyu mwanadada Batuli na mimi nikipitaga kwa blog yako nakutaga hayo majina anayoyapinga mtendee haki au hiyo mikataba ni urembo? Hujui kusoma? Marie Edward

    ReplyDelete
  3. Huyu ray tutaongea na CEO Sintah blog atuwekee tumvue nguo zote

    ReplyDelete