PENZI LA MUIGIZAJI AMANDA POSHY NA BWANA MISOSI LAOTA MBAWA.
Muigizaji Amanda Poshy na Bwana Misosi ambaye ni mwanamuziki wa Bongofleva wamemwagana huku baadhi ya watu wakidhani bado ni wapenzi. Alipoulizwa na Globalpublishers Amanda alikiri penzi lao kuota mbawa kwa kusema "Mimi na (Bwana) Misosi tumeachana muda mrefu tangu mwezi wa pili baada
ya kushindwana na katika uhusiano wa kimapenzi, nimejifunza kuwa
wanaume siyo watu wa kuwaamini asilimia mia moja kwani baadaye unaweza
kujuta"
Naye Bwana Misosi alipoulizwa kuhusu kumwagana na Amanda ambaye ni star wa filamu nchini alionekana kujikanyaga ikionekana hakutarajia habari hizo kuvuja kwenye media kuwa sio wapenzi tena " "Kwanza
niko safarini, je, ni nani aliyekuambia hizo habari….hebu ngoja
nimpigie huyo Amanda nimuulize nani aliyetoa siri hiyo"
Amanda Poshy
Like our facebook page Swahili World Planet
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.
No comments:
Post a Comment