Monday, July 29, 2013

ACTRESS SHAMSA FORD KUFUNGA NDOA MUDA SI MREFU.

Actress Shamsa Ford ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini anapanga kufunga ndoa hivi karibuni kwa mujibu wake mwenyewe ili kuishi pamoja rasmi na mchumba'ke wa siku nyingi kama mke na mume. Mchumba'ke anaitwa Dickson Matoke na wamezaa mtoto mmoja. Akizungumza na Globalpublishers Shamsa alisema "Nimeamua kufanya hivyo kutokana na namna baba wa mwanangu anavyoonesha upendo kwangu na hata kwa mtoto wetu (Terry), kwa kweli namshukuru Mungu nitakapomaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na muda si mrefu vikao vya harusi vinaanza" alipoulizwa kama baada ya kuolewa ataacha kazi yake ya filamu alisema "Mchumba'ngu ni mwelewa hana kizuizi katika kazi yangu ya sanaa cha msingi ni kutimiza wajibu wangu wa familia"

 All the best Shamsa
Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.





No comments:

Post a Comment