Pages

Tuesday, July 30, 2013

MODEL DAXX HANS AONYESHA MATUNDA YA KUWA SERIOUS KATIKA MODELLING.

Daxx Hans ambaye ni mwanamitindo maarufu wa kiume nchini akiwa anafanya kazi zake S.Afrika ameonyesha gari lake la rangi nyekundu kama linavyoonekana pichani amabalo analitumia akiwa Arusha katika mishe mishe zake anapokuwa nchini. Ukiachilia mbali hilo model huyo pia ana gari jingine ambalo lipo Dar es salaam na pia anajenga nyumba yote hayo yakiwa ni matunda ya kuwa serious katika tasnia ya mitindo ambapo alianzia hapa hapa nchini kwa muda mrefu na baadaye kupata deal S. Africa na tayari ameshatokea kwenye majarida maarufu na campaigns mbalimbali nchini humo kwa kipindi cha muda mfupi tu.

 Kwa hiyo wale models wa kitanzania ambao bado hawako serious na mitindo bali wanafanya kama sehemu ya kuuzia sura ni wakati wa kujua sasa kuwa tasnia hiyo inalipa vizuri sana kuliko hata kuwa meneja wa bank. Moja ya vitu ambavyo ni rahisi kumfikisha mbali zaidi Daxx ni kujiamini tofauti na models wengi nchini wakiwa hawana hali ya kujiamini na kutaka kuthubutu ili kufika mbali licha ya kuwa na vigezo vingine na hata Daxx mwenyewe alishawahi kukiri hilo. Ni kweli kupata channels ni ngumu kidogo lakini channels hizo hizo ili kuzipata ni lazima mtu kujiamini ili kudhihirisha kuwa unao uwezo wa kupambana na models wengine katika majukwaa ya kimataifa. Picha chini ni Daxx akiwa Arusha na mkoko wake ingawa tulishindwa kujua mara moja thamani ya magari yake.

Be inspired Tanzanian models
Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment