Serikali tayari imeshatoa tamko kuwa kufikia tarehe 1/7/ 2013 hakutakuwa na DVD
yoyote ambayo itaruhusiwa kuingizwa sokoni kama haitakuwa na stamp
ya TRA. Hatua hii ni katika kile ambacho wasanii na wadau wa filamu nchini wamejaribu kwa muda mrefu
kupigania na kupaza sauti zao katika kulinda haki zao za msingi hasa linapokuja suala la uharamia au piracy kwa lugha ya kiingereza. Matarajio ya wasanii wengi ni suala hili la stika kusaidia kwa
upande huo lakini inaonekana wazi kuwa bado nguvu za ziada zitahitajika katika kuondoa tatizo la uharamia wa kazi za sanaa nchini zikiwemo filamu kwakuwa stika pekee haziwezi kuondoa tatizo hili.
Jumatatu tarehe 3/6 pale BASATA kutakuwa na forum kwa ajili ya
kuzungumzia suala hili ambapo wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu,wasambazaji na
serikali watakuwepo.
No comments:
Post a Comment