Zitto Kabwe ameandika hivi katika facebook juzi ""Nollywood
has become the third-largest film industry in the world by value (US$
250 million per year) after Hollywood and Bollywood. It churns out 40
movies per week. It provides direct employment to an estimated 200,000
people, with another million jobs indirectly" - Ngozi Okonjo-Iweala,
Nigerian minister for Finance.
Tanzanian film industry is
second in Africa, but as a shadow minister for finance I can not give
figures, as the sector has been neglected. Reforming the sector through
formalization is paramount. We must be positive about our film industry,
it is a job creation machine. Issues of quality, copyrights and access
to finance must be addressed.".
Wengi wameonyesha wasiwasi kwa kuandika kuwa Tanzania ni ya pili baada ya Nollywood kama utafiti umefanywa au la!. Hao wameonyesha wasiwasi kuhusu ubora wa filamu lakini linapokuja suala la uzalishaji wa filamu kwa wingi Tanzania ni kweli inaelekea kuwa ya pili ingawa kunahitajika utafiti zaidi kwani hata katika ubora Tanzania yaweza kuwa juu kuliko baadhi ya nchi zinazotajwa kwa kukisia. Ghana bado haizalishi filamu nyingi sana na imejulikana haraka baada ya kuanza kushirikiana kwa karibu na Nigeria ingawa filamu zao ubora wao waweza kuwa juu kuliko zetu ingawa pia sio filamu zote.
Hata hivyo lengo la kuweka hii post ya Mh. Zito ni kuonyesha kuwa viongozi wanaanza kusapoti hii tasnia kwa mwanzo mzuri kama huu hivyo ni wajibu wetu wadau kufanya tafiti na viongozi waelezwe kwa kuwa wameanza kuonyesha nia ya kuisaidia tasnia ya filamu nchini. Tumpe zaidi sapoti Zito Kabwe na TAFF ni wajibu wenu huu pia kutoa ushirikiano maana kuna watu kama vile Bishop Hiluka ni watu muhimu sana katika hili ili kusaidia viongozi wa nchi kupata taarifa sahihi na hata ikiwezekana bajeti ya kufanyia tafiti iombwe kutoka serikalini.
No comments:
Post a Comment