Tuesday, May 14, 2013

WEMA SEPETU NA KAKA YAKE DIAMOND KUWA WAWAKILISHI WA BIG BROTHER AFRICA 2013 !

Habari za chini chini ni kuwa actress Wema Sepetu ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2006 yeye na Romeo Rommy Jones ambaye ni ndugu yake Diamond Platinumz ndiyo watakuwa wawakilishi wa Tanzania katika shindano maarufu barani Afrika, Big Brother Africa 2013(BBA) ambalo mwaka huu linaitwa " BBA The chase".Chanzo kimoja kimeitonya Swahiliworldplanet huku kikikataa kutajwa jina lake. Kimesema kuwa yeye ameambiwa na rafiki yake ambaye anafanya kazi DSTV lakini hakumhakikishia kwa asilimia zote huku akisita kuweka wazi na kubaki kucheka tu alipomuuliza kama Wema na Romeo ndiyo watakuwa wawakilishi. Ukiachana na chanzo hicho mtu mwingine jana aliambia Swahiliworldplanet kuwa alisikia mfanyakazi mmoja wa DSTV pia akitaja jina la Wema katika mazungumzo yaliyokuwa yanahusiana na shindano hilo lakini alishindwa kuyafuatilia kwakuwa alikuwa anaondoka na gari na kuwaacha waliokuwa na mazungumzo hayo. "t iz likly wema ndo ataend kula upepo BBA, i hed employee dstv aki-mention jina lake ktk talk related to bba bt nliondka na gari bila info ya ukwel ". kilisema chanzo hicho.

Wakati form za shindano hilo zilipotoka zilisambaa habari kuwa Wema alichukua form kwa ajili ya kujaribu bahati yake katika shindano hilo lakini  meneja wake Martin Kadinda alisema si kweli. Jana katika instagram Wema aliweka picha akiwa na Romeo ambaye wiki iliyopita habari zilianza kusambaa kuwa yeye ndiye mwakilishi wa BBA mwaka huu lakini mwenyewe alipoulizwa na gazeti moja alibaki kucheka tu huku ikidaiwa kama alikuwa akificha kitu chenye ukweli ndani yake. Inadaiwa Wema na Romeo wameanza kuwa karibu kwa ajili ya issue hiyo na chanzo hicho kikidai kuwa hata safari ya Wema kwenda Dodoma akijitia kudai maslahi ya wasanii ni moja ya mipango yake ili apate kura za watanzania akiwa mjengoni huko S. Afrika. Hata hivyo inadaiwa DSTV hawapo tayari kuweka jina la mwakilishi mpaka siku ya ufunguzi rasmi wa shindano hilo mwezi huu kuku ikidaiwa kuwa baadhi ya nchi zitatoa mwakilishi zaidi ya mmoja kwakuwa wanatakiwa wawakilishi 28 huku nchi zinazoshiriki zikiwa 14 au kila nchi kutoa wawakilishi wawili. Je hii ni kweli au uvumi tu? lets wait n see

                                                                 Wema Sepetu

No comments:

Post a Comment