Friday, May 10, 2013

WASICHANA WENGI WAMTAKA SLIM OMAR KIMAPENZI MPAKA AAMUA KUJITOA FACEBOOK KWA MUDA.

Slim Omar muigizaji anayezidi kujipatia umaarufu kila kukicha amekiri kuwa wasichana wengi wanamsumbua wakimtaka kimapenzi lakini yeye huwa anaona kawaida tu na anaepuka kuwajibu vibaya kwakuwa wao ni binadamu na wana matamanio na hisia pia. Aliongeza kuwa anashindwa kuwajibu vibaya kwa kuwa ndiyo mashabiki wa filamu zake. Amesema hata facebook ameamua kusitisha akauti yake kwa muda tatizo likiwa hilo pia lakini ataifungua tena muda si mrefu.

 Slim aliyasema hayo baada ya Swahiliworldplanet kumuuliza kuwa hapati usumbufu kutoka kwa wasichana baada ya kuwa maarufu na ni kwanini akaunti yake facebook haipo kwasasa?, ndipo alipofunguka muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto unaowadatisha wanawake wengi wa mjini. Alisema kuwa baadhi ya watu wanatumia vibaya mitandao ya kijamii wakati inatumiwa na watu wa rika zote."ntarudi 2 ndugu yangu nimetoka kwa muda maana kuna baadhi ya kina dada walikuwa wanai2mia vbaya kama unavyojua mitandao ya kijamii wanatazama wa2 wa kila rika na usumbufu upo kwa kna dada na ngumu kuzuia hisia zao na vibaya kuwajibu maneno mabaya ndo maana nimejitoa kwa muda ila ntarudi soon"

Muigizaji huyo anaonekana katika filamu kama vile Waves of Sorrow, I am Lost, Family War, Kivuli na nyinginezo huku filamu zake nyingine mpya zikitarajiwa kuwa sokoni muda si mrefu.


No comments:

Post a Comment