Pages

Saturday, May 4, 2013

THEN & NOW: WEMA SEPETU

Kama ilivyo kawaida binadanu hubadilika katika mambo mengi maishani wakiwemo mastaa wa kada mbalimbali. Katika Then & Now leo ni kwa Wema Sepetu. Kuanzia harakati zake za Miss Dar Indian Ocean, kutwaa taji la Miss Tanzania 2006 mpaka sasa star huyo amepitia mabadiliko mbalimbali. Kwanza umaarufu wake umezidi kuongezeka huku ukichochewa na skendo za mara kwa mara hasa maisha yake ya kimapenzi na mastaa wenzake. Baada ya kuvua taji lake la miss Tanzania ambalo ndilo hasa lililoanza kumpa umaarufu kama warembo wengine Wema alijitosa kwenye filamu kwa ushawishi wa marehemu Steven Kanumba. Ni star mkubwa sana kwa sasa pengine kuliko wenzake wote kwenye burudani lakini uigizaji wake ukiwa wa kawaida tu. Filamu zake zinauzika kutokana na kuwa na damu ya kupendwa huku acting skills zake zikiwa normal. Wema ana damu ya kupendwa sana na pia baadhi ya waliomkaribia na kujenga nae urafiki wameishia kuwa maarufu kupitia mgongo wake licha ya huko mwanzoni kabla ya kuwa karibu na Wema wakijaribu kufurukuta bila mafanikio kupitia vipaji vyao. Kingine kinachoonyesha mabadiliko ya star huyo ni rangi yake ya ngozi kutoka kuwa na mrembo mwenye ngozi halisi ya kiafrika mpaka kuwa na ngozi nyeupe kutokana na vipodozi alivyoamua kutumia kitu ambacho kimefanya kuwa hot topic kwa fans wake. Also umbo lake la kimis limepotea na kuwa na umbo la kibantu linalodatisha wengi. Wema pia amejizolea sifa nzuri kutokana na kusaidia wenzake katika matatizo akiwemo Kajala. Aangalia picha za mlimbwende huyo from Then and Now......................

 Mpaka kufikia alipo sasa kiumaarufu na muonekano Wema alianzia mwaka 2006
                             Siku alipotwaa taji la Miss Tanzania 2006
                                          alipokuwa akitupa karata zake Miss world 2006
Picha kutoka katika filamu ya "Red Valentine" moja ya filamu zake za mwanzo kabisa
                              Akiwa na Jumbe aliyewahi kuwa mpenzi wake
                          katikati ya mwaka 2012 katika uzinduzi wa filamu ya superstar
                                                                 Now


No comments:

Post a Comment