Sunday, May 12, 2013

SWAHILIWOOD BEST SCREEN MOTHERS

Leo ni siku ya mama duniani(Mothers Day) katika kukumbuka mchango wa mama katika kada mbalimbali hasa katika familia. Katika filamu za kiswahili pia mama wamekuwa na mchango mkubwa sana na bila wao hakuna mastaa wanaocheza nafasi za uhusika ukuu kama watoto au vijana. Mastaa vijana ndiyo wanaandikwa sana kwenye media hasa magazeti kuliko hawa mama ambao hucheza kama wazazi wao ili kufanikisha malengo ya kufikisha ujumbe na katika kufikia malengo yao katika maisha ya kila siku kutokana na jinsi story ya filamu ilivyoandikwa. Kama walivyo katika maisha yao halisi kwa kuonyesha tabia mbalimbali pia hata katika screen/ filamu wamekuwa wakionyesha tabia nzuri kama walezi wazuri wa watoto wao na kutoa ushauri mzuri, kuwa na hasira kwa watoto wao, roho mbaya na kadhalika. Here are some of talented mothers in our movies hasa katika filamu walizocheza kama mama bora na washauri wazuri kwa watoto wao.

1. Bi. Fetty
She is one of the most talented screen mothers in Swahiliwood. one of her memorable roles is in the film HATIA in which she played Hisani Muya's(Tino) mother. familia yake ilikuwa masikini sana huku mwenyewe akiwa mgonjwa lakini anampa mwanae ushauri mzuri kuhusu maisha na asikate tamaa. Licha ya kuwa na kipaji kikubwa lakini bado anaonekana kwenye filamu chache sijui kwanini watayarishaji wa filamu hawamtumii kwenye filamu zao na wakati mwingine wakiweka mtu anayeshindwa kuuvaa uhusika wa mama

2.Fatma Makongoro(Bi. Mwenda). anajulikana sana kwa kucheza uhusika wa roho mbaya lakini pia amecheza filamu nyingine katika positive characters na kufanya vizuri sana kama mama kuliko wengi waliocheza nafasi hiyo katika nafasi ya mama bora. She is a talented  screen mother in Swahili films.
3.Grace Mapunda
she is talented and has appeared in many films as a mother. She looked best in Kalunde. Cutt Off  and many more films. katika filamu ya HIT BACK kuna scene mwanae anafundwa mguu na gari na kulia kwa uchungu sana, scene ile ni moja ya scene ambazo si rahisi kusahaulika katika filamu za Swahiliwood katika kuonyesha mapenzi ya mama na mtoto.
4. Chuma Suleiman(Bi. Hindu)
Wengi hupenda lafudhi yake na uongeaji wake. amecheza filamu nyingi na kuuvaa vizuri uhusika wa mama.
5.Suzana Lewis(Natasha)
Amecheza filamu nyingi kama mama wa mastaa wengi huku akicheza pia kama mama wa mwanae halisi Yvone Cheryl(Monalisa) katika filamu kadhaa na kuuvaa vizuri uhusika.

6. Tecla Mjata.
She is a veteran actress akiwa na historia ndefu katika sanaa ya maigizo na filamu. amecheza kama mama wa wasanii maarufu akiwemo marehemu Steven Kanumba .
7.Farida Sabu
amecheza filamu nyingi kama mama wa mastaa wa Swahiliwood na kufanya vizuri sana.
8.Hidaya Njaidi.
Vicent Kigosi na Marehemu Steven Kanumba ni miongoni mwa watoto wa Hidaya Njaidi katika filamu za kiswahili.
9.Husna Poshy(Dotnata)
amecheza katika filamu nyingi kama mama nafasi hiyo akianzia katika kundi la mambo hayo na kumkaa vizuri.
Hao ni baadhi ya mifano mizuri ya mama bora na kutoa mchango mzuri katika filamu za kitanzania ingawa wapo wengine.

                                                           Happy Mothers Day



No comments:

Post a Comment