Ruge Mutahaba ameamua kumjibu Lady Jaydee katika mkorogano wao na Clouds
fm kuhusu suala la muziki wa Bongofleva, hata hivyo licha ya watu wengi
kusoma na kusikia alichokisema Ruge kuhusu Jay Dee na muziki wa
Bongofleva kwa ujumla asilimia kubwa ya watu mpaka sasa katika mitandao
ya kijamii wanaonekana kuwa upande wa Jaydee na kuamni alichokisema huku
madai na majibu ya Ruge yakishindwa kupewa uzito na wadau. Pia Jay dee ameahidi kuanika mambo mengine muda si mrefu. Katika ukurasa wake wa facebook ameandika hivi "
Kama
mtakumbuka niliahidi kutoa awamu ya pili tar 15 au 17 May na ahadi ni
deni..Japo naona mbali ila Nitafanya hivyo, bado nina mengi sana ya
kuzungumza kuhusu Ruge na wenzake...Ile ilikuwa ni trailer tu, Movie
ndio linaanza sasa #TeamAnaconda no surrender". Katika ukurasa wa Bongo5 facebook wachangiaji wengi pia wameonekana kuwa upande wa Jaydee baada ya habari ya Ruge kumjibu Jaydee kuwekwa. Angalia twitter nako hawapo nyuma.............
No comments:
Post a Comment