Pages

Saturday, May 4, 2013

RAYUU KUTESA AFRICA MAGIC NA SERIES YA HIGH HEELS.

Tuesday Kihangala ambaye huko nyuma alishatesa na tamthilia kadhaa kama vile Jumba La Dhahabu kwasasa anakuja na series nyingine kwa jina la High Heels ikiwashirikisha mastaa kibao waliotamba na Jumba la Dhahabu. Rayuu pia ni mmoja wa waigizaji na amepewa nafasi kubwa katika character yake. High Heels itarushwa hivi karibuni katika kituo cha Africa Magic Swahili. Mr.Chuzi pia ameshatoa filamu kadhaa kupitia kampuni yake ya filamu. Rayuu mwenyewe alipoulizwa na Swahiliworldplanet kuhusu ujio wake huo hakuwa na la ziada zaidi ya kusema mashabiki wake wasubiri wakitarajia makubwa katika tamthilia hiyo. Kaa mkao wa kula kwa ajili ya series hiyo.


No comments:

Post a Comment