Pages

Wednesday, May 1, 2013

MTOTO WA CHUCHU HANS AJITOSA SWAHILIWOOD NA KUONYESHA KIPAJI CHA KUIGIZA.

Farihiya ambaye ni mtoto wa actress maarufu wa Swahiliwood Chuchu Hans anadaiwa kuwa na kipaji kikubwa kwa mujibu wa waandaji wa filamu ya Wrong Hope chini ya Rj Company huku Johari akiwa Producer wa Filamu hiyo inayoongozwa na Juma Chikoka(Chopa) aliyekiri kuwa mtoto huyo ana kipaji kikubwa. Wakizungumza na thesuperstarstz walisema kuwa Farihiya ana kipaji na uwezo mkubwa wa kushika script haraka kitu ambacho kimeanza kuwafanya baadhi ya producers kutaka kufanya nae kazi. Mtoto huyo mwenyewe alisema kuwa anapenda kuigiza lakini shule ndicho kipaumbele chake cha kwanza na atafanya filamu tu katika muda ambao hauingiliani na shule. Chuchu Hans alisema kuwa anampenda sana mwanae na amefurahi kurithi kipaji chake lakini anahakikisha shule ikiwa kipaumbele kwanza huku akimpa malezi mazuri. The film also stars Blandina Chagula(Johari), Nurdin Momamed(Chekibudi) and Stanley Msungu. Mtoto huyo anafuata nyayo za waigizaji wengine Swahiliwood walioanza kuigiza tangu utotoni kama vile Elizabeth Michael(Lulu), Diana Kimaro na wengineo kitu ambacho ni cha kawaida hata Hollywood na Bollywood baadhi ya mastaa wakubwa leo walianzia kuigiza tangu utotoni. Look at the promising child actress akiwa location..............................

                                                    akiwa location na Chekibudi

                                                             images by thesuperstarstz

No comments:

Post a Comment