Habari ni kuwa Ritha Pauslen maarufu kama Madam Ritha ana mpango wa kuingia Swahiliwood kama film producer kupitia kampuni yake ya Benchmark Productions inayoandaa Bongo Star Search. Chanzo cha kuaminika na kilichokataa kutajwa jina lake kimeiambia Swahiliworldplanet kuwa Madam Ritha anataka kuingia kwenye filamu kama producer na miezi ya hivi karibuni amekuwa akijipanga ili kufanikisha malengo yake hayo lakini hana haraka kwa kuwa anataka kutengeneza filamu nzuri zitakazoleta mapinduzi ndani na nje ya nchi. Chanzo hicho pia kimesema kuwa Madam Rita anataka kufanya kazi na wataalam wa filamu waliosomea mambo hayo huku wengine wakiitwa kufanyiwa usaili wakiwemo wengine kutoka Kenya.
Kama Madam Rita kweli anangia kwenye filamu basi kampuni yake itakuwa moja ya kampuni zinazotarajiwa kuleta ushindani katika kuzalisha filamu na hivyo kupelekea ushindani wa kuzalisha filamu nzuri zaidi kwakuwa kampuni yake ni lazima itakuwa imejipanga vizuri hasa katika suala la mtaji ambalo bado ni tatizo kwa watengeneza filamu wengi nchini. Hatukufanikiwa kumpata Madam Rita ili kujua maoni yake lakini tukimpata tutakuletea yaliyo upande wake.
No comments:
Post a Comment