Chanzo cha kuaminika kimesema kuwa muigizaji Jackline Wolper amehamia kwenye nyumba mpya tena nzuri na yeye ameenda nyumbani kwa actress huyo. Chanzo hicho ambacho hakikutaka kutajwa jina lake kilisema kuwa Wolper mwenyewe amebaki kucheka kutokana na habari zilizoandikwa kwani amehamia katika nyumba nzuri na ya kisasa. Leo mitandao kadhaa imeripoti kuwa Wolper alitupiwa virago na mwenye nyumba wake kwa kushindwa kulipa kodi zaidi ya Millioni 2 lakini habari ni kuwa actress huyo alitaka kuhama katika nyumba hiyo huku baadhi ya walioulizwa wakisema ni kweli katupiwa virago. Chanzo hicho kilisema "mwenyewe anacheeka wakati kahamia kwenye nyumba mpya nzur tena apartment" chanzo hicho kiliiambia Swahiliworldplanet.
No comments:
Post a Comment