Pages

Thursday, April 4, 2013

RAY HATARINI KUPOTEZA NYWELE KICHWANI.

Muigizaji maarufu wa Swahiliwood Vicent Kigosi(Ray) anasemekana kuwa hatarini kupoteza nywele zake kichwani au kuota upara mapema kutokana na matumizi ya mara kwa mara ya kutumia mafuta ya kulainishia nywele kichwani ambayo wataalamu wanasema yana athari kwa mtumiaji kwa kuwa hutengenezwa kwa kemikali. Picha za hivi karibuni alizopigwa Ray akiwa katika harusi ya Kupa na Jimy zimemuonyesha Ray akiwa katika muonekano tofauti kuashiria kuwa wanachosema wataalam hao ni kweli. Nywele za Ray zilionekana kama mtu mgonjwa vile badala ya kupendeza kama lilivyokuwa lengo lake, muigizaji mmoja aliyekuwa katika harusi hiyo alipoulizwa alisema itakuwa ni hayo mafuta anayoweka mara kwa mara labda yameanza kumkataa. alisema "labda wave zmeanza kumktaa, cwajua pia kapungua uzito". Daktari mmoja alipoulizwa na SWP alisema mafuta hayo yana kemikali ambazo husababisha nywele za mhusika kukosa nguvu yake ya asili,kupoteza nywele mapema, kuota upara mapema na sababu nyingine zikitajwa kuwa ni kusababisha ugumba kwa mhusika. SWP ilipomtumia ujumbe Ray kuhusu muonekano wa nywele zake na walichosema wataalam hakujibu mpaka tunaandika habari hii.

Miaka ya hivi karibuni vijana wengi wanaojiita wa kisasa wamekuwa wakitumia mafuta hayo wengine huita wave ili kuwa watanashati wakiiga wenzao wa marekani lakini inadaiwa kuwa mafuta hayo mengine huwa fake ambayo ni hatari zaidi. Angalia picha Ray aliyopigwa wiki ilopita.


No comments:

Post a Comment