Monday, April 1, 2013

MAMA LORAA ATOA MSAADA KITUO CHA YATIMA, BABY MADAHA, SNURA NA FLORAH MVUNGI WAJITOSA KUWAPIKIA WATOTO HAO YATIMA.

Mama Loraa ambaye ni mfanyabiashara mkubwa, mdau na mlevi wa sanaa hasa ya filamu nchini jana alitoa msaada katika kituo cha watoto yatima kiitwacho New Life kilichopo Kigogo jijini Dar es salaam. Katika tukio hilo aliambatana na Swahiliwood actresses ambao ni Florah Mvungi, Snura Mushi and Baby Madaha ambao pia ni singers. Kina Baby Madaha ndiyo waliwapikia watoto hao chakula cha sikukuu ya Pasaka na kujumuika kula nao hivyo kutoa taswira nzuri kwa jamii wao kama watu maarufu na kioo cha jamii ambapo wengine wanatakiwa kuiga. Pia walitoa zawadi nyingine kwa kituo hicho kama sabuni, mafuta ya kupikia, unga na mchele. Hongera sana mama Loraa na actresses hao kwa moyo wa upendo na kukumbuka wasiojiweza. Angalia picha

 Mama Lora, Baby Madaha na Snura
                                                             wakigawa msosi
                                                      

No comments:

Post a Comment