Baadhi ya makampuni makubwa huwa yanatumia watu wasio na vigezo katika matangazo yao makubwa, lakini baadhi ya kampuni zipo makini katika matangazo yao zikiamua kuwapa kipaumbele wanamitindo. Matangazo ya Perone Beer yamewatumia wanamitindo wa Tanzania Richa Adhia ambaye pia ni Miss Tanzania 2007, model wa kiume Lota Mollel na Nelly Kamwelu ambaye pia ni Miss universe Tanzania. Kwa hapa nchini kinywaji hicho kutoka Italy kipo chini ya Kampuni ya Serengeti. Billboard mbalimbali zimewekwa wanamitindo hao wakionekana and nafikiri pia wamelipwa vizuri. Huu ni wakati muafaka makampuni mengine makubwa nchini kutumia wanamitindo wa nchini wenye vigezo na siyo kila mtu hata wasio na sifa.
No comments:
Post a Comment