Wednesday, April 3, 2013

LADY JAY DEE AWAGEUZIA KIBAO LINAH NA BEN POL KUWA WAMEKATAZWA NA BOSI WAO WASI-PERFORM NYUMBANI LOUNGE.

Baada ya kutoa makavu mazito mazito kwa Clouds fm kwa kutokupiga nyimbo zake mpya, safari hii Lady Jay Dee amewageukia wasanii wawili Ben Pol na Linah kuwa walikatazwa na bosi wao ku-perform Nyumbani Lounge siku ya Valentine Day. lady Jay Dee pia amebainisha kuwa show hiyo haikuwa yake bali kuna mtu alikodi ukumbi huo na wanamuziki hao wawili kutakiwa kutoa show huku wakipewa advance kabisa lakini walijitoa hatua za mwisho wakidhani ni show yake hivyo kumuangusha mwandaaji wa show hiyo. Jay Dee amesema kuwa wengi wanadhani anayoyazungumza na kuandika siku za hivi karibuni ni kuhusu nyimbo zake kutokupigwa pekee wakati yapo mengi likiwemo hili. Baada ya kuandika hivyo Ben Paul alimjibu Jay Dee. Angalia tweet zote hapo chini


No comments:

Post a Comment