Pages

Wednesday, April 3, 2013

IRENE UWOYA NA NDIKU WARUDIANA ! WAONYESHA MAHABA UKUMBINI.

Mwishoni mwa wiki iliyopita actress Irene Uwoya na aliyekuwa mumewe Hamad Ndikumana from Rwanda ambaye wanadaiwa kutengana walionekana kuwa na ishara ya kurudiana kwa kukumbatiana kimahaba bila wasiwasi huku wengi wakijua wapo kwenye gogoro zito. hivyo watu kuamini kweli wawili hao hawana bifu kama Uwoya anavyosisitiza mara kwa mara kuwa wapo poa tu kama zamani. Hayo yalitokea katika harusi ya actors wawili wa Swahiliwood Jimmy na Kupa. Chanzo makini kimeambia Swahiliworldplanet kuwa miezi ya hivi karibuni wawili hao wanaonekana kuwa karibu zaidi ikiwemo hivi karibuni kuwa wote katika tuzo za filamu nchini Rwanda. Hivyo kuna dalili labda wamerudiana lakini wengine hawajui,. Kwasasa Ndikumana anakaa kwao Rwanda akiwa star wa mpira wa miguu huku Uwoya akiwa Tanzania katika kazi zake za films. Licha ya wawili hao kudaiwa kutengana lakini bado Uwoya anapendwa sana nchini Rwanda kwa mashemeji na mawifi zake. Angalia picha hizo.................................


No comments:

Post a Comment