Mwanamuziki mkonge nchini Fatma Binti Baraka maarufu kama Bi. Kidude amefariki dunia leo hii, akizungumza na Bongo5 mjukuu wake aitwaye Omar alisema kuwa mwanamuziki huyo maarufu ndani na nje ya bara la Afrika alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya sukari na uvimbe katika kongosho hivyo alikuwa wakimrudisha kila mara hospitalini na leo hii mauti kumkuta. Mungu ailaze roho ya marehemu Bi. Kidude atakumbukwa vizazi na vizazi kwa kazi zake na kwa kukubalika kwa watu wa rika zote.
No comments:
Post a Comment