Pages

Thursday, April 25, 2013

BATULI AJUTA KUTUMIA KOPE BANDIA, ASEMA SIRUDII TENA ZIMENIPOTEZEA KOPE ZANGU ASILIA.

Actress maarufu wa Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli)anajutia kutumia kope bandia kwa kuwa zimemfanya kupoteza kope zake za asili na hivyo kukiri wazi kupitia facebook kuwa hatarudia tena urembo huo. aliandika " Kope sasa bhaaaasi, Nawaachia warembo...."
Swahiliworldplanet ilipomuuliza kama ni kweli alichoomanisha au anaigiza filamu mrembo huyo alisema ni kweli na hatarudia tena urembo huo ni hatari " Kope bandia sio nzuri zimefanya kope zng zikatike na kubaki chache sizitaki tena". tunampongeza sana Batuli kwa kukiri kosa alilolifanya na kujutia ili wanawake wengine wanaojifanya kwenda na wakati kwa kutumia urembo huo bandia wajifunze kupitia kwake maana yeye amegundua tatizo mapema kabla halijamuathiri zaidi.

Miaka ya hivi karibuni wanawake wengi wamekua wakitumia urembo wa aina mbalimbali ambao hudaiwa kuwa na madhara kwa mtumiaji lakini wengi huziba pamba masikioni kwa kutojikubali walivyoumbwa na Mungu. licha ya kope bandia kumfanya mtu ang'oke kope zake asilia, hudaiwa na wataalam kuwa humfanya mtu kope zake za asili zikose nguvu ya asili na pia zinadaiwa kusababisha upofu kwa mtumiaji, wengine pia huweka macho ya paka yanayodaiwa kuwa na madhara makubwa pia.



No comments:

Post a Comment