Tuesday, March 26, 2013

SWAHILIWOOD DIRECTORS AND PRODUCERS TUJIFUNZE HAPA KUPITIA RACHEL MWANZA.

Wakati nilipokuwa naangalia filamu ya Rebelle(War Witch) iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana na kupata tuzo kibao na pia kupendekezwa kama best foreign language film katika tuzo za Oscars/Academy Awards 2013,  actors walionivutia alikuwa Rachel Mwanza kutoka Congo ambaye ndiye mhusika mkuu na Serge Kanyinda who played supporting role akiwa na ulemavu wa ngozi(albino).  Rachel mwanza ambaye bado ni mtoto alifanikiwa kuuvaa uhusika vizuri  kwa kulazimishwa kuwaua wazazi wake na kuingizwa katika jeshi la waasi akiwa bado mtoto kiasi kwamba mara nyingi anasahau majukumu yake na akili zake za kitoto kumrudia, anakuwa mtumwa wa ngono na kupewa mimba na kiongozi wa waasi hivyo kupata mtoto huku yeye mwenyewe akiwa bado mtoto.Kupitia performance yake in this film Rachel amepata tuzo kibao kama best actress katika Berlin Film Festival, The Tribeca Film Festival, Vancouver Film Critics Circle and Canadian Screen Awards 2013. Rachel Mwanza ambaye amezaliwa mwaka 1997 alikuwa hajui kusoma wala kuandika alipofuatwa na director wa film hii Kim Nguyen na producer Pierre Even kwa kuwa alikuwa mtoto wa mitaani aliyetelekezwa na wazazi wake tangu utotoni hivyo hakwenda shule kabisa, Producers na director wa filamu hiyo now wanamgharamia ili apate elimu na sehemu nzuri ya kuishi mpaka akiwa mkubwa. Pia tayari Rachel ametokea katika film nyingne ya kinshasa Kids ambayo ni Belgian film.

Kilichonifanya niandike hapa ni kuwa wenzetu nje wapo makini sana na kazi zao kwa kuangalia kipaji na siyo kuangalia uzuri wa umbo na sura kwa muigizaji kama ilivyo kwa watengenezaji wengi wa films Tanzania wanaangalia sura na umbo bila kufikiria kipaji kwanza kama kipaumbele na ndiyo maana films nyingi hazina uhalisia kwa kuwa wanaocheza hawana vipaji au directors hawajui kazi hiyo. Watengenezaji wa film ya War Witch waliona kuwa Rachel ana kipaji na na anaendana na uhusika wa filamu licha ya kuwa hakujua kusoma wala kuandika tena akiwa mtoto wa mitaani but walitoka Canada kumfuata Congo baada ya kumuona katika documentary ya watoto wa mitaani. Leo hii Rachel Mwanza anajulikana mpaka Hollywood na dunia nzima. pia alipamba sana media mwaka huu katika tuzo za Oscars akiwa katika vazi la kitenge. Huu ni wito kuwa filamu ni kipaji na siyo uzuri wa sura wala umbo kwa kuwa films kibao za kitanzania hata kama story ni nzuri lakini zinakosa mvuto na ushawishi kwa kuwa actor husika hana kipaji. Tubadilike ili tufike mbali zaidi.

Rachel Mwanza and War Witch director Kim Nguyen at Oscars 2013
                                                     


No comments:

Post a Comment