Pages

Wednesday, March 13, 2013

RAY AINGIA GYM KUJENGA MWILI, WENGINE IGENI MFANO.

Baada ya kupungua ghafla na kudai kuwa amepungua kwa ajili ya film role na wadau kutokumuamini. Actor mwenye jina kubwa Swahiliwood Vicent Kigosi( Ray) ametoa picha zake akiwa Gym anakula chuma chini ya mtaalam wa mazoezi. Huo ni uamuzi mzuri sana kwa Ray maana kitambi alichokuwa amekiachia kichomoze kilimpotezea mvuto aliokuwa nao zamani. pia kama ameamua kufanya mazoezi basi ataonekana poa zaidi hata filamu zake zinazokuja maana huko nyuma baadhi ya films alizocheza hazikuendana na mwili wake.
Hongera sana Ray wengine igeni mfano huo mazoezi ni kitu muhimu na humfanya muigizaji acheze character yeyote ile hasa za ubabe. Pia tumeshuhudia waigizaji kibao wa nje wakiwa na miaka zaidi ya 40 lakini wakionekana bado vijana kabisa sababu ya kufanya mazoezi lakini kwa waigizaji wetu mtu ana miaka 25 lakini mh utadhani ana miaka 50. Hapa sio kwa waigizaji wa kiume pekee hata wa kike Gym inawahusu sana maana tumeshaona films kibao mtu anacheza kama polisi au character inamtaka atumie nguvu au kukimbia but dakika mbili tu anahema kama nini kwa kukosa pumzi. Mazoezi pia humfanya muigizaji awe na muonekano mzuri katika ngozi, afya na hata general appearance inakuwa ya kujiamini mbele za watu hasa kwa kuwa celebrities ni watu wanaokuwa mbele ya kadamnasi mara nyingi. jionee picha hizo Ray akitafuta six pack kwa udi na uvumba.






1 comment:

  1. If want to know more information on Muscles and Muscle gaining secrets then proceed to: www.somanabolicmusclemaximizereviewscam.com

    ReplyDelete