Pages

Monday, March 25, 2013

KAJALA AHUKUMIWA JELA MIAKA 5 AU KUTOA FAINI YA ML13, WEMA SEPETU AJITOLEA KUMSAIDIA.

Latest news ni kuwa Kajala Masanja who is a Swahiliwood actress amehukumiwa kwenda jela miaka 5 au kulipa faini ya shilingi mil 13 na mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu  katika kesi iliyokuwa inamkabili kwa muda sasa yeye na mumewe aitwaye Faraja Chambo. News ni kuwa actress Wema Sepetu ametoa kiasi kikubwa cha pesa ili kumsaidia Kajala . Wema alikwenda ATM kutoa pesa ili kumuokoa mwigizaji mwenzao.
Kajala na Faraja walikuwa wanakabiliwa na makosa matatu, kwanza ni kesi ya kula njama za kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es salaam kinyume cha sheria. Pili, ni kuwa April 14 mwaka 2010 walihamisha isivyo halali umiliki wa nyumba kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha sheria ya kupambana na rushwa ya mwaka 2007. Na shtaka la tatu ni la kutakatisha pesa ambalo walilitenda April 14 mwaka 2010 huku wakijua ni kinyume cha sheria. Mumewe amehukumiwa kwenda jela miaka 7 au kulipa faini ya shilingi mil 200. Tutakuletea habari zaidi ya kitakachoendelea endelea kusoma Swahiliworldplanet.
Hongera sana Wema Sepetu na Waigizaji wote waliojitoa ili kumsaidia mwenzao.

Wema Sepetu akiwa na kajala baada ya kulipa million 13.
                                                       Actress Kajala Masanja

3 comments:

  1. jaman mungu ambariki wema na wote waliijitolea kumtoa kajala

    ReplyDelete
  2. ATM za Tanzania unaweza to million 13 hiyo kiboko, hiyo kadi gani? Tembo

    ReplyDelete
    Replies
    1. c lazma Wema atoe mil13 directly coz hawez kosa akiba kwenye pochi so may be alikwenda toa za kuongezea tu ili ikamilike 13.

      Delete