Pages

Thursday, March 21, 2013

IRENE UWOYA ACHEMSHA KATIKA MAVAZI RWANDA MOVIE AWARDS.

Hivi karibuni actors wa Swahiliwood Vicent Kigosi(Ray), Irene Uwoya, Jacob Stephen and King Majuto walialikwa katika tuzo za filamu nchini Rwanda na kupewa heshima kubwa na hadhi ya kipekee kama mastaa wakubwa wa filamu. Hata hivyo siku ya utoaji wa tuzo hizo actress Irene Uwoya licha ya kuvaa gauni refu but halikumpendeza kama staa mkubwa mwalikwa katika tuzo hizo, pia aliharibu kabisa katika red carpet kwa kuvaa viatu flat aina ya loafer vya rangi ya blue kama gauni lake. Ukiongezea na pochi ndogo ya mkononi aliyokuwa amebeba aliishia kuonekana kama anakwenda sokoni kununua mahitaji ya nyumbani au anakwenda kwenye kikao cha Bongomovie!. Uwoya alitakiwa kuvaa viatu virefu(heels) katika event hiyo ya usiku. Pia angeweza kupendeza hata katika mavazi ya kifarika au mengine yenye asili ya kizungu but haikuwa hivyo. Pia kabla ya siku ya tuzo hizo walialikwa katika usiku wa siku ya wanawake duniani ambapo Jose Chamelione kutoka Uganda alitumbuiza but licha ya Uwoya kuvaa vizuri lakini aliharibu kwa kufungua vifungo vya gauni lake kifuani ili tattoo zake zionekane hivyo kuishia kuonyesha sehemu ya matiti yake kifuani kitu ambacho ni kosa katika fashion. Hii inaonyesha kuwa mastaa wetu wengi hasa wa filamu bado hawajajua wavae nini na wapi. Have a look...............

 alihojiwa na waandishi
Siku ya wanawake duniani alivaa hivi



No comments:

Post a Comment