Sunday, March 24, 2013

INTERVIEW WITH SWAHILIWOOD ACTOR STANLEY MSUNGU.

Kwa sasa huwezi kutaja waigizaji wanaotamba Swahiliwood then ukasahau kumtaja Stanley Msungu ambaye tayari ameigiza na wasanii mbalimbali wenye majina na wanaochipukia. Stanley ni mmoja wa actors wachache ambao wanacheza uhusika tofauti tofauti(versitile actor). kazi zake zinaonekana katika fims nyingi zikiwemo Stuck on You, Hit Back, Sweet & Scorpion na nyinginezo kibao. Stanley pia ni film star asiye na makuu na anayependa pia kukosolewa pale penye tatizo ili kuzidi kusonga mbele zaidi. Swahiliworldplanet ilimtafuta actor huyu kwa ajili ya interview kuhusiana na kazi zake za films so tiririka nayo hapo chini............

SWP: Mashabiki wako wangependa kujua ni lini ulianza uigizaji?

STANLEY: Sanaa nilianza miaka 6 iliyopita nikiwa na Amka Sanaa Group ambalo lilikua linaonyesha michezo yake ITV.

SWP: Unafikiri ni kwanini mpaka sasa filamu za kitanzania  zinahusu mapenzi kwa kiasi kikubwa wakati yapo mambo mengi ya kuzungumzia na kupendwa na mashabiki kuliko hata mapenzi?

STANLEY:  kwanza nakubali kuwa kuna vitu vingi vya kuzungumzia kwenye movie zaidi ya mapenzi ila hakuna chochote utakachozungumzia usiguse mapenzi, hata movie za wenzetu walioendelea ukuiangalia huwezi ukaangalia movie mpaka ikaisha bila kuona au kuzungumziwa mapenzi, hata hivyo sanaa yetu ndio inakua na sisi ndio tunaikuza tunatakiwa kupewa moyo zaidi.

SWP:  Je ni kweli kuwa wakati mwingine script katika filamu za kibongo inaweza kuwa nzuri lakini director akashindwa kufanya kazi nzuri sababu ya kutokuwa na uwezo wa kuongoza filamu?

STANLEY:  jibu ni kweli.

SWP: .Watu wanasema kuwa baada ya kifo cha Kanumba hakuna muigizaji yoyote wa kiume anayeonyesha juhudi za kuzitangaza filamu za kitanzania kimataifa kwa kutafuta soko na kucheza filamu na wasanii wa nje badala yake waigizaji wa kike hasa Lucy Komba na Yvonne Cheryl(Monalisa) ndiyo wanaosemekana kuwa na mtazamo wa kimataifa zaidi, je nini maoni yako?

STANLEY:  Hao wanaotafuta soko nje soko lao ndani likoje? jenga msingi ndani ndio utoke nje.

SWP:  Una ndoto za kufanya kazi na msanii gani wa filamu barani Africa na kwa nini awe huyo?

STANLEY:  Sina ndoto za kufanya kazi na msanii yoyote wa Africa ila nina ndoto za kufanya kazi nzuri na zenye ubora unaotakiwa ili hao wanaoitwa wasanii wakubwa Africa na nje ya Africa wanitafute.

Stanley with Nollywood superstar Ramsey Nouh
 SWP: Umecheza films nyingi sana and now wewe ni msanii mkubwa unayejulikana so unasaidiaje vipaji vichanga ili navyo vionyeshe uwezo wao?

STANLEY:  kwangu sina njia nyingine ya kuwasaidia wasanii wachanga zaidi ya kuwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwenye kazi zangu.

SWP:  Mavazi katika films nyingi za kitanzania ni moja ya matatizo makuu kiasi cha kuharibu story ya filamu na filamu husika, je ni kwanini hakuna muda wa kutafuta mavazi stahili wakati films nyingine mavazi yake sio gharama kuyapata?

STANLEY:  Muda wa kutafuta mavazi upo ila msanii mwenyewe huenda hajijui tu kuwa yeye ni nani na kazi anayoenda kuifanya hajaielewa.

SWP:  Ni muigizaji gani wa kike nchini ambaye ukiigiza nae pamoja mna-suit sana characters husika?

STANLEY: Irene Uwoya and Jackline Wolper.

SWP:  Unafikiri ni kwanini watengenezaji wengi wa films Tz hawana mwamko wa kupeleka films zao katika matamasha ya filamu mbalimbali wakati ni moja ya fursa nzuri ya kutangaza kazi zao kimataifa?

STANLEY:  Hawajiamini na pengine hawajui nini faida yake.

SWP:  Nini ushauri wako kwa serikali kuhusu kuinua tasnia ya filamu nchini?

STANLEY:  Hakuna kipya ni kutupia jicho tu kwenye sanaa.

SWP:  Waambie chochote mashabiki wa kazi zako.

STANLEY:  Mashabiki wangu na wa movie kwa ujumla napenda kuwaomba wasisahau tulikotoka na sanaa yetu, wasipende kukosoa tu hata mtu akifanya vizuri wawe wanasema pia na wasipende kusifia tu na tukikosea watuambie pia, kingine wajivunie kilicho chao.

                  ...............xxxxxxxxxxxxxxxxxxx..................................................

No comments:

Post a Comment