Thursday, January 17, 2013

HUYU NDIYE MSAMBAA ANAYETAMBA HOLLYWOOD

Wengi wakiwemo waigizaji wa kibongo hawamfahamu Rachael Zawadi Luttrell(41) ambaye alizaliwa nchini Tanzania.Ameshaigiza katika series na filamu kadhaa hollywood kama vile Stargate Atlantis(2004), The Aviary(2005),Everiday Use(2003) na nyinginezo. pia alifikiriwa kucheza katika filamu iliyotamba sana ya X-MEN katika uhusika wa storm. Muigizaji huyu alizaliwa Dar es salaam mama yake akiwa ni msambaa wa Lushoto bi Veronica Makihio na baba yake mzungu Dr. William Leon Luttrell. muigizaji huyu pia ni mwanamuziki na mwaka 2011 alitoa albamu yake ya jazz "I wish you love".Ameshaigiza filamu na series zaidi ya 20 huko hollywood za mwanzo zikiwa zimezalishwa nchini Canada.

No comments:

Post a Comment