Pages

Saturday, January 5, 2013

EXCLUSIVE INTERVIEW WITH ACTRESS LUCY KOMBA IN DENMARK

Waigizaji wengi wa filamu za kitanzania wanajulikana sasa lakini baadhi ya watu bado hawajui kuwa muigizaji Lucy Komba ni chachu ya kujulikana kwa wasanii hao kama vile Irine Uwoya. Lucy ni muigizaji mwenye kipaji na mara nyingi uigizaji wake ni natural tofauti na waigizaji wengi. Now yupo nchini Denmark akimalizia shooting ya filamu yake ambayo hakuitaja jina kutokana na sababu maalum. Tayari ameshaigiza filamu nyingi sana kama vile Familia yangu, Kipenzi Changu,Watoto wa Mjini, Pretty Teacher na nyinginezo. Lucy ni mmoja wa waigizaji wachache sana wa kitanzania ambao wameamua kuanza kulisaka soko la kimataifa na siyo kutegemea la Tanzania pekee kwani tayari ameshasafiri nchi mbali mbali kama vile Ghana, Nigeria, Denmark na nyinginezo ili kuangalia namna ya kupanua soko la kazi zake.She is busy in Denmark shooting for her upcoming film but bado alinipa muda kwa ajili ya mashabiki wake,ili kujua nini amekisema msanii huyu tiririka hapa chini.....
SWALI:Mashabiki wako wangependa kujua safari yako nchini Denmark ni ya kikazi au mambo binafsi tu?
LUCY:Nimekuja Denmark kwa ajili ya kujua hasa wenzetu wanafanyaje kazi zao na filamu zetu zinachukuliwaje huku, pia nimekuja kufanya filamu huku denmark?
SWALI:Je ni filamu gani kwa sasa una-shoot na humo ndani umeshirikiana na waigizaji wa Tanzania pekee au waigizaji kutoka nchi nyingine?
LUCY:Filamu ninayoitengeneza sasa nisingependa kuitaja jina ila baadaye mtaifahamu jina, hiyo filamu nimeshirikiana na watu kutoka Tanzania,Congo na Denmark.
SWALI:Miezi ya hivi karibuni tumeona ukiangalia soko la kimataifa zaidi kwa ajili ya kazi zako unaweza ukatueleza zaidi kilichokusukuma kufanya hivyo?
LUCY:Ni kweli naangalia sana soko la kimataifa kwa sababu nataka kujifunza na kutengeneza filamu zitakazopendwa kimataifa na nimebadilika kwa kweli filamu zangu zitakazotoka kwasasa zitakuwa tofauti kabisa, nimejaribu kubadlilisha uandishi wangu wa stori pia.
SWALI:Umetembelea baadhi ya nchi kadhaa mpaka sasa,je umegundua nini kuhusu filamu za kitanzania katika nchi ulizotembelea ikiwemo Denmark?
LUCY:Nimegundua kuwa filamu za Tanzania zinapendwa sana na watanzania wenzetu walioko nchi za nje ikiwemo huku Denmark lakini bado zinakosolewa sana kulingana na filamu za wenzetu wa nje.
SWALI:Umekuwa mstari wa mbele sana katika kuwasaidia wasanii wachanga waonyeshe vipaji vyao na wengine tayari ni mastaa wakubwa wa filamu kwa sasa, kati yao ni waigizaji gani watatu tu uliowasaidia kutoka ambao mpaka sasa unajivunia?
LUCY:Wasanii watatu ambao ninajivunia sasa ni Irene Uwoya, jackline Wolper na Ahmed Olotu(Mzee Chilo).
SWALI:Unatarajia kurudi Tanzania baada ya muda gani?
LUCY:Natarajia kurudi Tanzania hivi karibuni nitakapomaliza hii filamu ninayotengeneza.
After the interview www.swahiliworldplanet.blogspot.com wished our actress all the best.

No comments:

Post a Comment