Pages

Wednesday, December 19, 2012

WATENGENEZA FILAMU ZA KITANZANIA ACHENI KUIGA UNAIGERIA ISI NI ZAIDI YA WANAIGERIA IA

ubunifu katika filamu za kitanzania bado ni tatizo sana. Mara nyingi hata mavazi na make ups wanaiga kutoka Nigeria hasa kwa filamu zenye story za kiasili kitu ambacho kinapunguza hamasa kwa watazamaji wanaoona ni afadhali kuangalia filamu za kinigeria kuliko kuangalia za kitanzania. Hakuna shaka kuwa mazingira ya kiafrika yanafanana kwa namna moja au nyingine lakini bado kuna tofauti kutoka nchi moja na nyingine ikiwemo mavazi. Angalia hawa wabunifu wa kitanzania na kazi zao ambazo zinaweza kutumiwa hata na watengeneza filamu wa hollywood katika filamu zenye story za enzi za ujima au utumwa na nimekuwa nikijiuliza sana tatizo ni nini maana wabunifu hawa wanaweza kukodisha haya mavazi tena kwa bei ya kawaida tu kwa maelewano ya kikazi ila watengeneza filamu kama sio woga wa kuwafuata itakuwa tatizo ni nini?. nje baadhi ya filamu zinachukua hata miezi ili kutafuta vazi hata likiwa moja hasa kama ni la kifalme au vazi maalum ili kuendana na story husika, sasa hapa kwetu story ya enzi za ujima au utumwa muigizaji kavalishwa kaniki mpya au mavazi yenye asili ya Nigeria ikiwemo make ups ! angalia kazi za mbunifu Gabriel Mollel na Diana Magesa ni kiwango hata cha kutumiwa hata hollywood kwa story zenye asili ya kiafrika angalia mavazi ya DIANA MAGESA
angalia mavazi ya GABRIEL MOLLEL
mavazi yenye vionjo vya kimasai ni moja ya vitu vinavyotakiwa ili kututofautisha na Nigeria na hata kama wamasai wapo kenya sio tatizo bado tutaonekana watanzania na waswahili

No comments:

Post a Comment