Pages

Thursday, December 18, 2014

Wema Sepetu, Jokate Na VJ Penny Walikataa Kunizalia Mtoto: Diamond Platnumz

Diamond amefunguka baada ya kuulizwa amekuwa akitangaza kupenda watoto lakini kwa nini hana mtoto mmoja licha ya kuwa na uhusiano  na wanawake mbalimbali.
Akizungumza na Globalpublishers Diamond alisema: “Ni kweli napenda watoto lakini siwezi kupata mtoto peke yangu bila mwenzangu. Lazima kuwe na mwenzangu ambaye tutakubaliana.“Nilichojifunza ni kwamba wenzangu hawakuwa real (hawakumaanisha) hivyo wakawa wanachengachenga.”
Diamond aliendelea kueleza kuwa VJ penny aliwahi kupata ujauzito wake mara mbili ila ukatoka
 “Ukweli Penny ningezaa nae, aliwahi kuniambia ana mimba yangu, sikuamini, nikampeleka hospitali kupima ikawa kweli. Kesho yake niikamnunulia gari, nikamwambia mama tulia. Siku mbili tatu akasema mimba imetoka"
“Nikaja nikamjaza kingine cha pili (mimba), nayo baada ya muda akaja kuniambia imetoka. Nikaona huyu mzinguaji, nikammwaga. Lakini iliniuma sana.“Kwa wengine (Jokate na Wema) walikuwa wakinichenga tu bila sababu, unamuona huyu hataki kubeba mimba yangu. Mtu kwa mdomo anasema kwamba yuko na wewe kikamilifu lakini kwa matendo unaona siye"
“Lakini kusema ukweli kabisa natamani sana kuwa na mtoto.
“Hapo juzikati nilitaka kuoa, kila kitu kilikuwa sawa, nikaja kubadili mawazo.”
Swali: ”Ulitaka kumuoa nani?”Diamond: “Ah! Siwezi kumsema hapa"  Diamond alimaliza.

No comments:

Post a Comment