Pages

Friday, December 5, 2014

Wema Sepetu Afuatwa Agombee Ubunge 2015 Na Kuahidiwa Uwaziri !

Haya ni makubwa !...... Wema Sepetu anadaiwa kufuatwa na Waziri mmoja wa chama tawala ili agombee ubunge jimbo moja jijini Dar es salaam katika uchaguzi mkuu wa mwakani 2015 na kuahidiwa uwaziri pia.


 Kikizungumza na Swahiliworldplanet jana chanzo kimoja kutoka kwa Wema Sepetu kimesema kuwa Waziri huyo ambaye anatajwa katika mbio za kugombea urais 2015 anaona Wema anaweza kushinda Ubunge kwa jinsi alivyo na ushawishi na anavyopendwa na watu wa rika zote.

" Wema ameshafuatwa agombee ubunge hapa Dar es salaam  na waziri(akimtaja jina) isitoshe kaahidiwa uwaziri pia kama akiibuka kidedea, Wema ana ushawishi sana mpaka wanasiasa wakubwa wanamnyemelea, unajua Wema ana damu ya siasa baba yake siwajua alikuwa politician na mwanadiplomasia, lakini bado Wema hajaamua kama agombee au hapana" kilisema chanzo hicho huku kikitabasamu

Ukiachilia mbali Wema huko nyuma Jackline Wopler pia alidaiwa kuwa atakuwa waziri ikiwa Mgombea flani anayedaiwa kuwa na nguvu CCM atashinda urais !.

No comments:

Post a Comment